Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watu 187 wenye uzito mkubwa, wapunguzwa tumbo, mafuta

Dhambi Nchi Unene.jpeg Watu 187 wenye uzito mkubwa, wapunguzwa tumbo, mafuta

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)-Mloganzila, imekwishawafanyia upasuaji wa kupunguza uzito watu 187, tangu kuanza kwa huduma hiyo, Desemba, mwaka 2022.

Aidha, kati ya hao asilimia 80 ya waliofanyiwa upasuaji, wengine wamerekebishwa mfumo wa tumbo la chakula.

Profesa Mohamed Janabi, ametasema hayo leo, Dar es Salaam. “Tumewafanyia upasuji kwa makundi matatu.

“Kuna waliowekewa puto tumboni, wengine wamepunguzwa ukubwa wa tumbo na baadhi wamefanyiwa upasuaji wa kunyonya mafuta,” amesema Prof. Janabi.

Amesema Muhimbili itaendelea kuwajengea uwezo wataalam wake kwa kuwa, malengo kwa sasa ni kuifanya MNH-Mloganzila kuwa kituo cha umahiri huduma za upasuaji rekebishi kwa Ukanda wa Afrika Mashariki.

Prof. Janabi amesema hayo alipokutana na timu ya wataalam wa upasuaji kwa lengo la kuwashukuru na kuwapongeza kwa kufanikisha kambi ya upasuaji rekebishi iliyofanyika hivi karibuni, MNH-Mloganzila.

Kambi hiyo ilishirikisha wataalamu kutoka MNH Upanga na Mloganzila, Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), pamoja na mtaalamu mbobezi kutoka nchini India.

Prof. Janabi ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo, imekuwa na matokeo chanya, huku baadhi ya wagonjwa waliopata maradhi ya kisukari kilichosababishwa na uzito mkubwa, afya zao zimeanza kuimarika.

“Mbali ya kuwafanyia upasuaji, wamewapatiwa elimu ya chakula na wamebadilisha mtindo wao wa maisha, sasa wanakula chakula kidogo jambo ambalo linawasaidia kudhibiti hali ya sukari mwilini,” amesema Prof. Janabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live