Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Watoto wabainika korodani zao zinapanda

Janabi Pic Data Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi.

Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoto 10 wa Mkoa wa Arusha wamebainika korodani zao zinapanda badala ya kushuka chini jambo ambalo hawataweza kuwa na watoto watakapokuwa wakubwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi, aliyasema hayo jana wakati akiwahudumia wananchi waliojitokeza kupatiwa matibabu jijini Arusha.

Amesema kwa familia za watoto hao hawana uwezo watakusanywa na kusafirishwa pamoja kwa ajili ya matibabu ya upasuaji.

Janabi alisema kuna baadhi ya fedha za Rais Samia zilizobaki zitatumika kuwatibia watoto hao 10 na kurejea katika afya njema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live