Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wapenda betting, pombe hatarini kwenda Mirembe

Wapenda Betting, Pombe Hatarini Kwenda Mirembe Wapenda betting, pombe hatarini kwenda Mirembe

Wed, 12 Jun 2024 Chanzo: Ayo

Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Jijini Dodoma imesema zipo tabia nyingi kwenye Jamii ambazo Watu huzifanya zinazoashiria wana changamoto ya afya akili au magonjwa ya akili ikiwemo ku-bet, kunywa pombe na kutumia simu kupita kiasi, kutoridhika na kukosoa kila kitu, kuona kila Mtu ni mbaya na hakupendi, kutukana na kucomment vibaya mitandaoni, kuogopa kupanda ndege, lift n.k ambapo imesema Mtu akijiona na viashiria hivi anapaswa kuwahi Mirembe ili apewe ushauri au dawa badala ya kusubiri hadi apelekwe akiwa amefungwa kamba.

Akiongea na @AyoTV, Mtaalamu Bingwa wa Saikolojia na Afya ya Akili amesema;

“Kuhusu ku-bet Watu wanataka kuongeza kipato lakini Wataalamu wa Afya ya Akili tunajiuliza iweje Mtu afikirie maisha yake anaweza kumudu kwa kubahatisha?, Mtu huyu tunaanza kutilia mashaka akili yake, Mtu anachukua hela ya ada, mshahara wake wote kwenda kubet, kubobea kwenye ku-bet ni uraibu (addiction) na hawa pia tunawahudumia kama Warahibu wa dawa za kulevya”

“Pombe kupita kiasi ni tatizo mpaka Mtu akikosa pombe anatetemeka, Mtu kupata furaha kupita kiasi na akiwa na hela ananunua hata asivyohitaji na kutoa ofa kwelikweli ni tatizo, kuna Mtu kila Mtu ni mbaya anaona kila Mtu hampendi ofisini hadi nyumbani, una haja ya kuchunguzwa”

“Magonjwa ya akili yanazidi 300, kuna magonjwa ya wasiwasi ikiwemo Mtu ghafla anapata mshtuko moyo, kuogopa kusimama mbele za Watu kuzungumza, kuna Watu wanaogopa kupanda lift au kukaa vibaraza vya maghorofa pekee yao, uoga kupanda ndege, Mtu akipoteza hali ya kupenda vitu alivyokuwa akivipenda siku za nyuma mfano outing na ghafla anajitenga au kujiona hana thamani na hata kufikiria bora kufa, huu ni ugonjwa wa akili”

“Mtu anapojiona ana changamoto ni vizuri akaja Mirembe kuliko kufikiria wewe ni mzima ukabaki Mtaani halafu ukaletwa siku umefungwa kamba, kuhusu ubalozi tunatumia Watu wenye ushawishi kama Mh. Jokate ambao afya zao za akili zipo vizuri ili watusaidie kupeleka elimu kwenye Jamii kwahiyo sio kweli Mtu tunayemtumia akawa ana tatizo na hata walio-comment vibaya kuhusu ubalozi wa Mh.Jokate nao wanafaa kuchunguzwa afya yao ya akili, lindeni afya zenu za akili”

Chanzo: Ayo