Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wananchi wa Comoro sasa kutibiwa Benjamin Mkapa Dodoma

Wananchi Wa Comoro Sasa Kutibiwa Benjamin Mkapa Dodoma.png Wananchi wa Comoro sasa kutibiwa Benjamin Mkapa Dodoma

Wed, 4 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa Visiwa vya Comoro sasa watatibiwa nchini badala ya kufuata huduma hizo Ulaya na Mashariki ya mbali.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Comoro, Moustadroine Abdou ameyasema hayo alipotembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma leo ambapo alishuhudia huduma mbalimbali ambazo wananchi wa Comoro walikuwa wakizifuata Ulaya na Mashariki ya mbali.

"Huduma tulizokuwa tunazifuata Ulaya na Asia kama upandikizaji wa figo kumbe tunaweza kuzipata hapa Tanzania.” Alisema Spika Abdou akiwa hospitalini hapo.

aAkiwa hospitalini hapo spika huyo alitembelea idara za magonjwa ya moyo, huduma ya upandikizaji uloto (Tiba ya Sikoseli), idara ya dadiolojia (MRI), kliniki maalumu ya viongozi na wodi ya Rais.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Dkt Godwin Mollel amesema ziara hiyo imempa fursa spika Abdou kushuhudia mageuzi makubwa aliyoyafanya Rais Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Afya.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Kessy Shija amesema hospitali hiyo inahudumia zaidi ya wananchi milioni 14 katika Kanda ya Kati na mikoa ya jirani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live