Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WHO imeonya kuhusiana na ongezeko la maambukizi ya magojwa ya zinaa

WHO Imeonya Kuhusiana Na Ongezeko La Maambukizi Ya Magojwa Ya Zinaa.jpeg WHO imeonya kuhusiana na ongezeko la maambukizi ya magojwa ya zinaa

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SHARE Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani ni kwamba, watu zaidi ya milioni 1 huambukizwa magonjwa ya zinaa kila siku ikiwemo kaswende na kisonono.

Ongezeko kubwa zaidi la maambukizi limeshuhudiwa barani Amerika na Afrika.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa tahadhari kuhusu changamoto katika mapambano dhidi ya magonjwa ya zinaa.

Kulingana na taarifa ya iliyotolewa na WHO, idadi ya kila mwaka ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa kaswende iliongezeka kutoka karibu milioni 7.1 mwaka 2020 hadi milioni 8 mwaka 2022.

Jumla ya watu 230,000 walikufa kutokana na magonjwa ya bakteria mwaka 2022.

Magonjwa ya zinaa ni miongoni mwa maambukizi yanayofahamika sana na yaliyoleta madhara makubwa hasa katika nchi zinazoendelea ambazo nyingi ziko barani Afrika.

Ripoti hiyo pia iligusia kupungua polepole kwa maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU).

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kuwa, nchi nyingi tayari zimeendeleza mikakati ya kiafya ya kuzuia maambukizi ya VVU na kaswende kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live