Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usugu wa dawa za VVU waibua changamoto mpya ya matibabu

Usugu Wa Dawa Za VVU Waibua Changamoto Mpya Ya Matibabu.png Usugu wa dawa za VVU waibua changamoto mpya ya matibabu

Fri, 13 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Asilimia 5.8 ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi (waviu) na wanaotumia dawa, wanakabiliwa na tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo, utafiti mpya umeonyesha.

Usugu wa dawa dhidi ya vimelea vya magonjwa ni changamoto kubwa inayoikabili dunia kwa sasa.

Lakini usugu wa virusi vya Ukimwi (VVU) dhidi ya dawa za kufubaza makali ya ugonjwa huo, yaani ARV ni changamoto mpya kwa wanasayansi, wakiwa bado hawajapata suluhu ya tiba ya ugonjwa huo.

Usugu wa dawa ARV pia umetajwa kuwaathiri wenye maambukizi mapya, ambao wamekuwa wakipata changamoto wanapoingizwa katika matibabu.

Kisayansi, virusi vinapojenga usugu dhidi ya dawa za ARV, maana yake ni kuwa hazitaweza tena kupambana na VVU, hivyo kuendelea kuzaliana na kinga za mgonjwa ‘CD4’ kushuka na hatimaye ataanza kupata magonjwa nyemelezi, yaani Ukimwi.

Utafiti uliotolewa hivi karibuni na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), ulionyesha asilimia 5.8 ya waviu na wanaotumia dawa, wanakabiliwa na tatizo la usugu wa vimelea dhidi ya dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo.

Mtafiti Mwandamizi Kitengo cha Maikrobaiolojia na Kinga MUHAS, Dk Doreen Kamori, anasema walifanya utafiti huo mwaka 2020 katika mikoa 22 Tanzania Bara, ikiwamo Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe.

Dk Kamori anataja sababu zinazochangia tatizo hilo ni pamoja na kuingizwa nchini dawa ambazo zinachangia usugu na watu kutokuwa wafuasi wazuri wa kutumia dawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live