Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ummy azindua kambi ya madaktari bingwa wa Samia

Ummy 7c676d638 Ummy azindua kambi ya madaktari bingwa wa Samia

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ya huduma za afya nchini, upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa, na kuongeza wataalamu wa sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya nchini

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango kabambe wa kambi ya ‘Madaktari Bingwa’ wa Rais Samia unaolenga kufikia Hospitali zote 184 za Halmashauri nchini, hafla iliyofanyika kwenye viunga vya Hospitali ya Manispaa ya Iringa (Frelimo) kitaifa leo, Jumatatu Mei 06.2024 ambapo amesema mpango huo unalenga kutimiza dhamira na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan unaokusudia kuona Watanzania wanapata huduma bora za afya nchini

Waziri Ummy amesema mpango huo unalenga kubadilishana ujuzi, na uzoefu baina ya ‘Madaktari Bingwa’ wa Rais Samia na Madaktari wanaowakuta kwenye Hospitali za wilaya lengo likiwa ni kuhakikisha baada ya Madaktari hao kuondoka waache alama ya kufanyika kwa zoezi endelevu kwenye sekta hiyo

Sambamba na hilo amesema mpango huo unalenga kusaidia Hospitali za wilaya kuanzisha, na kusaidia uanzishwaji wa wodi maalumu za watoto wachanga (siku 0 hadi 28), kuanzisha vifaa visaidizi vya kusaidia watoto wachanga kupumua jambo ambalo ameagiza Halmashauri mbalimbali nchini kufanikisha ununuzi wa vifaa hivyo ili kwa pamoja kusaidia kuokoa maisha ya watoto wachanga pale wanapopata matatizo hayo

Amesema serikali ya awamu ya sita (6) inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imefanikisha kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa zaidi ya asilimia 80 lakini, bado kuna changamoto kwenye vifo vya watoto wachanga kwa kuwa vimepungua kwa asilimia nne (4) pekee hivyo ni wakati muafaka sasa kila mmoja kwa nafasi yake kuunga mkono juhudi za Rais Samia kuhakikisha vifo vya watoto wachanga vinapungua kwa kiasi kikubwa, kwa kuwa Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema uwepo wa wodi maalumu ya watoto wachanga unapunguza vifo hivyo kwa zaidi ya asilimia 50 .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live