Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ugonjwa wa monkey pox DR Congo ni 'hatari zaidi'

Aina Mpya Ya Ugonjwa Wa Monkey Pox Nchini DR Congo Ni 'hatari Zaidi'   Wataalamu Aina mpya ya ugonjwa wa monkey pox nchini DR Congo ni 'hatari zaidi' - Wataalamu

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Aina mpya ya virusi vya mpox inayosambaa kwa haraka katika mpaka wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo "inatia wasiwasi sana", wanasema maafisa wa afya wanaofuatilia kuenea kwake.

Virusi hivyo, ambavyo vinaweza kusababisha vidonda kwenye mwili mzima, vinawafanya baadhi ya watu kuwa wagonjwa sana na kuwaua.

Mlipuko wa sasa umechangiwa na maambukizi kupitia ngono lakini kuna ushahidi kwamba aina hii ya ugonjwa pia inaweza kuenezwa kupitia mgusano kimwili kati ya watu.

Wataalamu wa afya duniani wanasema aina hiyo mpya ya virusi inaweza kuvuka mpaka na kuenea kimataifa, huku mmoja akiitaja kuwa " bado ni zaidi bado".

Janga la dunia la mpox mnamo 2022 lilidhibitiwa kwa kuwachanja watu walio hatarini kuambukizwa.

Lakini upatikanaji wa chanjo na matibabu nchini DR Congo bado ni changamoto na maafisa wa afya nchini humo wanaonya kwamba virusi vinaweza kufikia nchi zingine.

"Ugonjwa unaweza kupitia viwanja vya ndege. Mtu mwenye vidonda anaweza kupitia mipakani kwa sababu hakuna udhibiti," alisema Leandre Murhula Masirika, afisa mkuu wa idara ya afya katika jimbo la Kivu Kusini - moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi nchini DR Congo.

Chanzo: Bbc