Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Misri kushirikiana sekta ya Afya

Ummy 7c676d638 Tanzania, Misri kushirikiana sekta ya Afya

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tanzania na Misri ziliingia mkataba wa makubaliano kati ya Wizara ya Afya na Shirika la ALAMEDA Healthcare Group Oktoba, 2022 ili kushirikiana katika nyanja ya Afya hasa upande wa huduma za kimatibabu kwa kubadilishana uzoefu, usimamizi wa hospitali na matibabu ya wagonjwa wa Kimataifa.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameeleza hayo jana Aprili 29, 2024 kwenye kikao chake cha kwanza na Balozi wa Misri nchini Tanzania Sherif Abdelhamid Ismail kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma.

“Ni furaha kwetu kuendelea kushirikiana katika kubadilishana wataalamu wa Afya, kubadilishana teknolojia na programu za mafunzo na elimu, kubadilishana madaktari, wauguzi, mafundi wa radiolojia, mafundi maabara pamoja na wanasayansi wa tiba.” Amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amemuomba Balozi huyo kusaidia wahudumu wa Afya ya Jamii (CHWs) watakao ajiriwa 137,000 wenye jukumu muhimu la kutoa huduma za Afya kwa watu ambao hawajafikiwa.

Kwa upande wake Balozi za Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Nchini Tanzania, Sherif Abdelhamid Ismail amemshukuru Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa kumkaribisha na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live