Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saratani yaua watu 27,000 kila mwaka nchini

#LIVE: Ummy Mwalimu Anasoma Muswada Wa Bima Ya Afya Kwa Wote Bungeni Saratani yaua watu 27,000 kila mwaka nchini

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kati ya Watanzania 40,000 wanaogundulika kuugua saratani 27,000 hupoteza maisha kila mwaka huku viashiria vikionesha vifo hivyo huwenda vikaongezeka mara mbili iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa ifikapo mwaka 2030.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa takwimu hizo hii leo jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa kituo cha huduma za saratani chini ya Hospitali ya Aga khan.

Amesema saratani inayoongoza ni ya mlango wa kizazi kwa asilimia 23.5 hali inayoifanya Serikali kuchukua hatua za makusudi ikiwemo kushirikiana na wadau mbalimbali ili kupambana na ugonjwa huo unaochangia kupotea kwa nguvukazi za taifa. - Naye, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati, Dk Doto Biteko akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho amesema serikali imejidhatiti kuimarisha ushirikiano na wadau wa sekta mbalimbali nchini ili kuboresha huduma za kijamii ikiwemo afya ili kuongeza weledi na kuboresha utoaji wa huduma hizo hali itakayosaidia kuongeza kasi ya maendeleo endelevu ya taifa - “Serikali imejipanga kuboresha huduma za afya na kupambana na magonjwa yasiyoambukiza, tayari serikali imetenga eneo kilipojengwa kituo hiki ambacho kimepanga kuhudumia wagonjwa 100 kwa siku kwa matibabu ya mionzi, wagonjwa 25 kwa siku kwa tiba za kemikali na wagonjwa 25 kwa siku kwa uchunguzi wa saratani na huduma za chanjo,” amesema Biteko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live