Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu wajawazito kuvimba uso, miguu hizi hapa

Mimba D Watoto Sababu wajawazito kuvimba uso, miguu hizi hapa

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miongoni mwa mambo yanayojitokeza kwa baadhi ya wajawazito katika kipindi cha miezi minne mpaka tisa, ni kuvimba pua, uso na wengine miguu.

Catherine Malya ni miongoni mwa wanawake waliobadilika mwonekano katika kipindi cha ujauzito wake.

"Nilivimba mwili mzima, pua ilikuwa kubwa, mdomo na uso vyote vilivimba, nilibadilika sana. Kitu pekee mume wangu alinisihi nisiwaze kuhusu hali hiyo, alinipa ujasiri sana," anasema Catherine, mkazi wa Mbezi Beach, jijini Dar es Salaam.

Simulizi hii inafanana na ile iliyoandikwa Desemba 16, 2022, mwanadada kutoka Uganda, Heyosato aliyeweka mitandaoni picha yake iliyoonesha mabadiliko ya mwili wake yaliyosababishwa na ujauzito wake.

Picha hiyo ilisambaa kwa kasi mitandaoni na ndani ya muda mfupi, wanawake kutoka mataifa mbalimbali walitoa shuhuda zao namna walivyobadilika baada ya kupata ujauzito na ilifikisha wafuatiliaji milioni 7.3 kwa saa chache.

Hata hivyo, wataalamu wa afya ya mama na mtoto wanasema changamoto kama hii huwakumba wanawake wengi na ni dalili ya changamoto kadhaa, ikiwemo matatizo ya figo na kifafa cha mimba vinavyoweza kumkuta mjamzito.

Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi, Isaya Mhando anasema mara nyingi hali kama hii inaweza kuwa ya kawaida kwa mjamzito kumkuta.

Anasema mjamzito anapobeba mimba ili mtoto aweze kulishwa vizuri kwenye mji wa mimba, lazima presha ya damu inayopita kule iwe ndogo ya chini, ili kuruhusu virutubisho vya chakula na oksijeni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa urahisi.

Dk Mhando anasema maji yanayotengeneza damu huongezeka kwa asilimia 30 hadi 50, hiyo ndiyo huitwa hali ya kawaida ya ujauzito. Na wajawazito hawa huvimba miguu, uso na wakati mwingine pua au mdomo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live