Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpango wa chanjo ya malaria mbioni kukamilika

Malaria Malariaa.png Mpango wa chanjo ya malaria mbioni kukamilika

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema iko mbioni kukamilisha matumizi ya chanjo ya Malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini ambayo iliidhinishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) mwaka 2022/2023.

Akizungumza wakati wa Mkutano wa kwanza wa Mwaka wa tathmini ya ufanisi wa viashiria muhimu chini ya Wizara Mpango wa Malaria,Kifua kikuu na ukoma na Virusi vya Ukimwi na Homa ya Ini, Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria, Dk Samwel Lazaro amesema chanjo moja tayari imeshasajiliwa nchini.

"Sisi kamanchi tuna utaratibu wa kuhakikisha chanjo zinatumika na hadi sasa chanjo moja imesajiliwa ya R21 na Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba ( TMDA) hatua inayofata ni kupelekwa kwa timu ya wizara ya afya ili iweze kupitiwa namna gani itatolewa na kwa utaratibu upi.

Ameongeza "Ikiwa tayari wizara itaona namna ya kuanza utekelezaji wa utoaji. Amesema serikali imepiga hatua ambapo mpaka sasa maabukizi ya Malaria ni asilimia 8.1 na kwa miaka 10 wamekuwa chini ya asilimia 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live