Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkojo kutumika kupima TB

Sa Tb Mkojo kutumika kupima TB

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Afya nchini imesema inakusudia kuanza kutumia mkojo kwa watoto badala ya makohozi ili kutambua maambukizi ya kifua kikuu kwa kundi hilo.

Mkuu wa Programu hiyo kutoka Wizara ya Afya, Dk Catherine Joachim amesema katika mkutano wa mapitio ya programu za nusu mwaka kwa Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na homa ya Ini (NASHCOP), Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP), na Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma (NTLP).

Amesema tayari mashine za upimaji mkojo zimeshaanza kutumia kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.

"Sasa teknolojia imekua kama nchi tumeleta teknolojia hiyo ya kutumia mkojo na tumeanza baadhi ya maeneo kupima watoto kifua kikuu kwa njia ya mkojo na changamoto itafika mwisho sasa tunafikiri kupata vitendanishi vya kupima,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live