Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhagama: Mgonjwa ahudumiwe saa zisizozidi tatu

P 1Waziri Mhagama Ahimiza Ubora Mnara Wa Mashujaa Mhagama: Mgonjwa ahudumiwe saa zisizozidi tatu

Wed, 21 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri mpya wa Afya, Jenista Mhagama amezitaka Hospitali zote na vituo vya Afya Nchini kuhudumia Wagonjwa wa nje wanaofika kupata huduma kwa saa zisizozidi tatu.

Waziri Jenista amesema hayo jana August 20, 2024 wakati alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General) ili kuona hali ya utoaji wa huduma sambamba na kuongea na Watumishi waliopo Hospitalini hapo.

Amezitaka Hospitali zote Nchini na kuziagiza kuzingatia mzunguko wa utoaji wa huduma kwa Wagonjwa na kuhakikisha mzunguko huo unatumia saa za kitaalamu ambayo hazizidi tatu kwa kila Mgonjwa na kupunguza muda wa Wagonjwa kukaa Hospitali kusubiri huduma.

“Mgonjwa anapofika katika kituo cha afya au Hospitali asianze kuwaza ameenda kukaa sehemu hiyo kwa siku nzima na hivyo kusitisha shughuli zake nyingine, zingatieni mzunguko mzima wa utoaji huduma kwa Wagonjwa kwa kuzingatia muda wa utaalam usiozidi saa tatu, muda huo ni kuanzia Mgonjwa anapofika Hospitalini kwa kuanza kujiandikisha, kumuona Daktari, wakati anapatiwa matibabu na kupatiwa dawa”

Ili kufanikisha hilo Waziri Mhagama amesisitiza uwepo wa matumizi ya TEHAMA pamoja mifumo kusomana ikiwa njia ndiyo njia pekee ya kuokoa muda na kutoa huduma bora kwa Mgonjwa ikiwa ni sehemu ya kupunguza malalamiko ya mara kwa mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live