Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matumizi akili bandia: Dkt. Yonazi akutana na Wataalam

Screenshot 20240510 071410 PixelLab Matumizi akili bandia: Dkt. Yonazi akutana na Wataalam

Fri, 10 May 2024 Chanzo: dar24

Katika kuangalia uwezekano wa matumizi ya akili bandia kufanya mapitio ya matumizi ya umma, Serikali imefanya mazungumzo na Wataalam kutoka Oxford Policy Management.

Mazungumzo hayo, yamefanyika ya Wataalamu hao na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi ofisini kwake jijini Dodoma.

Dkt. Yonazi amesema pia lengo la mazungumzo hayo ni kujadili kuhusu makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto nchini. kufuatia Serikali ya Tanzania kuzindua Programu ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM), mwaka 2021.

Uzinduzi huo ni mpango mkuu wa kuzileta pamoja Wizara na wadau mbalimbali, ili kuboresha makuzi na maendeleo ya awali ya Watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka 8.

Chanzo: dar24