Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madaktari Bingwa kuwafuata wagonjwa Wilayani

Madaktari Madaktari Bingwa kuwafuata wagonjwa Wilayani

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na changamoto wanazokutana nazo wagonjwa kusafiri umbali mrefu kuwafata madaktari bingwa wa Mama Samia wanaokuwa wameweka kambi katika hospitali za rufaa, Uongozi wa mkoa wa Morogoro umeanza zoezi la kusambaza madaktari bingwa katika Hospitali saba ndani ya wilaya ili kuepusha adha hizo kwa wananchi.

Madaktari hao bingwa 35 wa Mama Samia wanasambazwa katika hospitali za Halmashauri saba mkoani Morogoro kwa ajili ya kuwafikia wagonjwa wanaoshindwa kumudu gharama za matibabu pamoja na nauli ili kuepusha vifo huku kila hospitali ikipatiwa madaktari bingwa watano watakaohudumia kwa siku tano kuanzia Juni 3 hadi 7 mwaka huu.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima ameipongeza Serikali kwa kuongeza jitihada katika Sekta ya afya kwani imepunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

"Kuanzia miaka ya 2015/2020 tumetoka kwenye vifo 556 kwa wakina mama laki moja hadi kufikia 2022 kuwa na vifo 104 ni sawa na 81% hii ni kwa mujibu wa ripoti ya viashiria vya afya ya uzazi (TDHS).

Katika hatua nyingine Waziri wa katiba na Sheria Mhe Pindi Chana ameeleza matibabu ni muhimu kisheria na kuwataka wananchi kufanya uchunguzi (Check up) ya miili yao mara kwa mara ili kujikinga zaidi.

Naye, Ismail Mtitu Mwakilishi kutoka wizara ya Afya amesema madaktari hao watatibu magonjwa ya uzazi, magonjwa ya watoto, magonjwa ya ndani,magonjwa ya ganzi pamoja na magonjwa ya mifupa.

Joyce Gimonye ni miongoni mwa daktari bingwa wa Mama Samia kutoka Geita ameeleza wamepokea maagizo hayo ya kusambazwa katika hospitali za Halmashauri ndani ya mkoa huo yakiwa na lengo la kusaidia wagonjwa kuepukana na vifo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live