Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kimarika huduma za ukunga kutapunguza vifo vya uzazi

Ummy 7c676d638 Kimarika huduma za ukunga kutapunguza vifo vya uzazi

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imedhamiria kuendelea kuboresha huduma za Ukunga pamoja na kuongeza idadi yao ili kupunguza vifo vya watoto wachanga.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hayo kwenye Siku ya Mkunga Duniani akisisitiza kuwa sio kila mtu anaweza kufanya kazi ya Ukunga, "kwani ni taaluma ambayo tunataka tuendelee kuitambua zaidi na wakati umefika wa kutofautisha uuguzi na ukunga."

Aidha, Waziri Ummy amesema wakunga wamekuwa msaada mkubwa kwenye kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga ambapo afua nyingi za afya za uzazi na mtoto zinaendelea kuboreshwa ili kutoa huduma bora za uzazi na afya ya mtoto.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewataka wakunga kuendelea kuwahudumia wateja kwa kutambua wajibu wao wa kuimarisha afya zao ili kufanikisha Dira ya 2025 ya Tanzania na Mendeleo Endelevu yenye malengo kupitia utoaji wa huduma ya afya ya uzazi inayokidhi mahitaji ya afya ya uzazi kwa wanawake na vijana.

Siku ya Mkunga Duniani huadhimishwa kila Mei 5, na kwa mwaka huu nchini maadhimisho hayo yamefanyika mkoani Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live