Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

KCMC wampongeza Rais Samia kwa jambo hili

Kmc Msz KCMC wampongeza Rais Samia kwa jambo hili

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chuo cha Afya cha KAM College kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu ya sekta ya afya nchini ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba ikiwemo MRI na CT SCAN kwa hospitali za ngazi ya wilaya na mikoa.

Akitoa pongezi hizo, Mkurugenzi wa Chuo hicho, Dkt. Kandore Musika amesema uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali ya awamu ya sita ni ushahidi wa dhamira ya Rais Samia ya kuipeleka mbele sekta ya afya ikiwemo maboresho ya sera ya elimu ikiwemo maboresho kwenye mitaala ya elimu nchini.

“Tayari Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTIVET) limekuruhusu kuanza kwa udahili kwa wanafunzi wa mwaka wa masomo wa 2024/2025 na hiyo inaenda sambamba na maboresho ya mitaala ya elimu hususani kwenye eneo la kupata ujuzi.” Amesema Dkt. Musika.

Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa ubora wa miundombinu ya afya nchini unasaidia kwa kiwango kikubwa kusogeza huduma za afya karibu na wananchi hivyo kusaidia kupata matibabu badala ya kwenda umbali mrefu.

“Mbali na wananchi kupata huduma bora pia wanafunzi wanaohitimu KAM College hupata nafasi za ajira kwa wepesi kutokana na kuongezeka kwa fursa za ajira.

"Wahitimu wa kada kama vile utabibu, maabara, ukunga, meno, rekodi za afya, sayansi ya fya ya mazingirana famasia na kozi za VETA wanaotoka KAM College wamekuwa wakipata ajira haraka katika taasisi za umma na taasisi binafsi na hili ni lazima tumpongeze Rais Samia”. Amesisitiza Dkt. Musika

Chuo hicho cha sayansi ya afya kilichoko Kimara Korogwe, Dar es Salaam kimefungua udahili kwa wanafunzi wa ngazi za Astashahada na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2024/2025 baada ya NACTIVET kutangaza kufungua dirisha la usajili wa wanafunzi wapya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live