Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

JKCI yazindua mtambo wa kisasa wa Oksijeni

Jkci.jpeg JKCI-DAR GROUP yazindua mtambo wa kisasa wa Oksijeni

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

: TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)–Hospitali ya Dar Group leo imezindua mtambo wa kisasa wa kuzalisha hewa ya oksijeni wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 500, utakaopunguza gharama za ununuzi wa oksijeni kutoka katika vituo vingine.

Mtambo huo umenunuliwa nchini Uturuki na kukabidhiwa kwa JKCI-Dar Group na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) ambapo kiasi cha Sh milioni 320 zilitumika kwaajili ya ununuzi wa mtambao na Sh milioni 70 kwaajili ya kasha la kuhifadhia mtambo, usafirishaji na Sh milioni 136 kwaajili ya kusimika na kusambaza hewa wodini na sehemu nyingine zenye uhitaji.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk Delila Kimambo amesema mtambo huo unatumia umeme na kuzalisha hewa ya oksijeni yenye ujazo wa milimita za mraba 21 yenye kasi ya mita tano kwa saa wakati wa kujaza.

“Una vifaa vingi ndani yake vikiwemo kifaa cha kupima ubora wa oksijeni, kifaa cha kujaza hewa, tanki la kupokea hewa ina lita 1000 na talinalopokea hewa ya oksijeni wakati wa kutoa lina lita 1000,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live