Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hospitali ya Chato kuanza upasuaji wa moyo

Chatooo Hospitali ya Chato kuanza upasuaji wa moyo

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali Wilayani Chato Mkoani Geita inatarajia kuanza ujenzi wa jengo kubwa la upasuaji wa moyo na mishipa ya damu ifikapo mwaka 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato ambapo itawasaidia Wananchi kutosafiri tena hadi Dar es salaam kwa ajili ya kupata huduma hizo za upasuaji katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato Husna Abdallah amesema hayo akiwa katika maandalizi ya kuwapokea Madaktari Bingwa na Bobezi wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu katika Hospitali hiyo kuanzia July 15 na 17 mwaka huu.

Husna amesema huduma hizo zitahusisha uchunguzi wa huduma za matibabu ya magonjwa ya Presha , Kisukari , magonjwa ya moyo pamoja na mishipa ya damu huku Wataalamu wakitumia nafasi hiyo kuwapa elimu ya tiba ya lishe bora ambayo itawasaidia Wananchi wa kanda hiyo kuepukana na magonjwa hayo.

Amesema lengo la uwanzishwaji huduma hizi katika Hospitali ni kuwanusuru Wananchi wa Kanda ya Ziwa ikiwemo Geita , Kagera , Mara ,Shinyanga , Simiyu na Mikoa ya Jirani pamoja na Nchi za Jirani kama Burundi , Rwanda na Uganda kuondokana na vifo vinavyosababishwa na magonjwa hayo kukithiri.

Zaidi ya Wananchi 3400 tayari wametibiws na kupimwa na kati yao Wananchi 576 wamegundulika kuwa na matatizo ya presha , kisukari na magonjwa ya moyo ambapo walipatiwa matibabu na wengine kutibiwa huku wakiwa chini ya uangalizi wa Madaktari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live