Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu faida za muhogo kiafya

Mihogo Mzdz Fahamu faida za muhogo kiafya

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukitembea katika jiji la Dar es Salaam,na Mwanza anakoishi be Faida potea mojawapo ya vitu utakavyoviona barabarani ni pamoja na wanawake wanaouza mihogo mibichi. Wauzaji hawa huwalenga sana wanaume na vijana.

Wakati wa janga la Uviko 19 na matatizo ya kiuchumi, Rais Yoweri Museveni wa Uganda aliwataka watu wake kugeukia mlo wa mihogo kama mbadala wa kupanda kwa bei ya ngano wakati ambao gharama ya maisha duniani kote ilipanda.

Muhogo ni chakula muhimu duniani. Barani Afrika ni muhimu zaidi kwa kuwa muhogo unaweza kupandwa katika udongo ambao hauna rutuba nyingi na hata katika eneo ambalo halina mvua ya kutosha.

Zao hilo linalostahimili ukame pia linatajwa kuwa na faida za kiafya. Muhogo unaelezwa kuwa na virutubishi vingi. Ni chakula namba tatu kwa wanga baada ya mchele na mahindi.

Mihogo inaweza kuliwa kama kisabeho Jules Kouassi, Daktari wa Afya ya Umma na mtaalamu wa lishe, kutoka Ivory Coast, anasema muhogo ni chakula muhimu, kwa sababu unaweza kuliwa na kila mtu na kuna njia tofauti za kutayarisha chakula hicho.

Anasisitiza, kwa vyovyote vile unavyotaka kuandaa muhogo, unapaswa kukumbuka muhogo hauliwi mbichi, kwa sababu una kemikali ndani yake.

Anasema unapaswa kuupika muhogo kwa usahihi. Kwani sio tu mizizi yake ndio yenye faida, hata majani ya muhogo pia yana faida.

''Majani na miziz yana vitamini A, B, C, E kwa wingi - pia hutoa virutubisho vingine kama vile magneshiamu, maadini ya chumvi, chuma na kalshiamu,'' anasema Dkt. Kouassi. Kuna wanga mwingi kwenye muhogo - ni kama 70% ya muhogo ni wanga, kwa hivyo hufanya mwili kuwa na nguvu za kutosha,” anasema Dkt. Kouassi.

Muhogo una faida sana kwa watu wanaofanya kazi nzito ambayo hutumia nguvu nyingi," anasema Dkt. Kouassi.

“Muhogo pia husaidia kupambana na shinikizo la damu mwilini na itakusaidia kulala vizuri. Hii ndiyo sababu watu wengi Afrika, wanapomaliza kula muhogo, husema wanataka kulala."

Kulingana na Dkt. Kouassi, majani ya muhogo yanafaa kusaidia kupambana na upungufu wa damu au ukosefu wa seli nyekundu za damu.

Lakini kwa kuwa kuna mihogo ambayo ina kemikali inayoitwa cyanide ndani yake, ni muhimu kuipika kwa muda mrefu ili kemikali yote itoke.

"Ni lazima uupike vizuri. Na kuumwaga maji," anasema Dk. Kouassi.

Mitindo ya upishi wa muhogo Majani ya muhogo yaliyotwangwa huliwa kama mboga na chakula kingine Lakini pia muhogo unaweza kutumika kutengeneza chakula kingine. Unga wa muhogo hutumika kutenegeneza ugali, vipopoo, keki, uji, mandazi na mitindo mengine mengi ya upishi.

Sandrine Tchoni kutoka jiji la Douala, nchini Cameroon anasema, huchemsha muhogo kisha hula na chakula maarufu Afrika Magharibi cha okok.

Katika maeneo ya Afrika Mashariki, hasa maeneo ya pwani – muhogo wa kuchemsha mara nyingi huliwa na kitoweo cha samaki.

Pia mtindo mwingine maarufu wa kupika muhogo, ni ule kuukata kata vipande vidogo baada ya kuumenya kisha hupikwa na nazi na baadae huliwa na samaki.

Kwa wanafunzi wa shule muhogo huula ukiwa umekaangwa. Na mara nyingi huliwa na chumvi pembeni au kachumbari.

Pia katika nchi nyingi za Afrika. Majani ya muhogo hupondwa yakiwa mabichi na hupikwa na tui la nazi na kuwa mboga – ambayo unaweza kula hata na wali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live