Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Energy drink, nguvu za kiume kufanyiwa uchunguzi

Nguvu Za Kiunme.jpeg Energy drink, nguvu za kiume kufanyiwa uchunguzi

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi Bilioni 3.5 kwa ajili ya kufanya tafiti kwenye maeneo sita ya sekta ya afya nchini.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hayo Mei 13, 2024 Bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha hoja ya bjaeti ya makadirio, mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Waziri Ummy amesema ili huduma za afya ziendelee kuimarika nchini ni lazima ziende sambamba na kufanyika kwa tafiti zitakazotoa majibu ya ushahidi wa kisayansi.

Ummy ametaja maeneo yatakayoguswa kwenye tafiti hizo ni pamoja na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo saratani, ufuatiliaji wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa, changamoto ya afya ya akili, Matumizi ya ‘Energy Drink’, nguvu za kiume na dawa za tiba asili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live