Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajabu! Friji ya nyumbani yahifadhi damu hospitali

Damu Friji Aaaii (600 X 319) Ajabu! Friji ya nyumbani yahifadhi damu hospitali

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais - TAMISEMI Dk. Rashid Mfaume ametaka utaratibu wa haraka uchukuliwe kuwezesha Hospitali ya Halmashauri ya Mji Korogwe Magunga kupata jokufu maalumu la kihifadhia damu baada ya kubaini matumizi ya jokofu la nyumbani hospitalini hapo.

Akiwa katika ziara ya usimamizi shirikishi katika mkoa wa Tanga amebaini jokofu la matumizi ya nyumbani likitumika kuhifadhia damu katika Hospitali ya hiyo na kuonesha kutoridhishwa na kitendo hicho.

"Hili jokofu ambalo mnatunzia damu ni kama tulilolikuta kule na hii tumeletewa na mdau lakini ni jokofu la mbogamboga kama mchicha. Tumetoka kule Shinyanga Mwalugulu tumewasema tukajua huku mmejifunza mtahangaika na sisi hatutaki kuona haya yanayofanyika huku tuyaone sehemu nyingine lakini mnaonekana Korogwe TC mnawataalamu wa kununua domestic friji … Tumeenda maabara pia tumekuta majikofu sita yote Domestic (ya majumbani)," amesema Dk. Mfaume.

Mwezi Aprili 2024 wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika mkoa wa Shinyanga timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI ilibaini ukiukwaji ma manunuzi ya majikofu ya kuhifadhia damu katika kituo cha Afya Mwalugulu kilichopo halmashauri ya Msalala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live