Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika kusubiri kwa muda mrefu kupata chanjo ya mpox

Afrika Kusubiri Kwa Muda Mrefu Kupata Chanjo Ya Mpox.png Afrika kusubiri kwa muda mrefu kupata chanjo ya mpox

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: Bbc

Nchi za Afrika ambazo zimeathirika na mpox zitalazimika kusubiri muda mrefu zaidi kupata chanjo hiyo.

Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, Afrika CDC, vinasema imeweka mpango wa bara hili kukabiliana na ugonjwa huo ili upata chanjo mwezi Septemba.

“Tunataka kuweka juhudi zetu zote sehemu moja. Afrika itakuwa na mpango mmoja wa kukabiliana na mpox na bajeti moja. Tunataka kuimarisha uwezo wa nchi kutumia chanjo hizo zitakapopatikana," Dk. Jean Kaseya, Mkurugenzi Mkuu wa Afrika CDC alisema.

Hata hivyo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kitovu cha mlipuko huo, haitapokea michango iliyoahidiwa ambayo ilitarajiwa wiki hii.

Nigeria ilipokea dozi 10,000 za chanjo ya Bavarian Nordic, Jumanne -msaada kutoka Marekani.

Nchi hiyo ilikuwa imeanza mchakato wa kupata chanjo hizo hata kabla ya mpox kutangazwa kuwa dharura ya kiafya duniani.

Vikwazo vya udhibiti na changamoto za manunuzi zimesababisha kuchelewa huko.

Afrika pia inataka kupata chanjo zake kama bara na sio kama nchi moja moja.

Chanzo: Bbc