Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Waitara awaita waastafu kwenye gofu

Golf Waitara Waitara awaita waastafu kwenye gofu

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashindano ya kila mwaka ya NBC Waitara Trophy 2024, inaendelea kwenye Viwanja vya Lugalo, jijini Dar es Salaam, huku Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali George Waitara ameyazungumzia mashindano hayo, huku akiwaita wastaafu wenginje kujumuika pamoja kusaidia mchezo wa Gofu.

Jenerali Waitara amesema mashindano hayo yaliyoanzishwa mwaka 2007 amesema yanazidi kukuwa na kuongezeka ubora na kufichua kabla hajastaafu, alikataza mashindano hayo kuitwa kwa jina lake (Waitara Trophy) badala yake alitaka yaendelezwe mashindano ya CDF, lengo lilikuwa kila kiongozi anayekuja aendeleze.

"Nadhani waliniogopa wakati sijastaafu, baada ya kustaafu nikakuta wenye klabu wanayaandaa ya Waitara Trophy, niseme nafurahi kuona yanafanyika kila mwaka na yanakuwa mazuri zaidi," amesema Jenerali Waitara na kuongeza

"Haya mashindano ni mazuri, kwani ni mahali pazuri pakutukutanisha wastaafu baada ya kutoka makazini,pia yanawakutanisha watu mbalimbali wa nyanja tofauti, hivyo ni muhimu waje kwani pia ni afya kwao."

Mashindano ya CDF ni Kombe la Mkuu wa Majeshi yanayofanyika kila mwaka, ndio maana alisisitiza yaendelezwe ili kila mkuu anayekuja ayasimamie.

Jenerali mstaafu Waitara kwenye kundi lake alilocheza nalo leo, alikuwa na viongozi wengine Edmund Mdolwa, Balozi Ombeni Sefue na Balozi Charles Sanga.

Chanzo: Mwanaspoti