Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Wadau waitwa kujiandikisha gofu 2022

Cleze Pic Data Wadau waitwa kujiandikisha gofu 2022

Fri, 21 Jan 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wachezaji wa klabu mbalimbali za mchezo wa gofu nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kushiriki shindano la 'Waitara Johnnie Walker Trophy' linalotarajiwa kufanyika Januari 29 jijini Dar es Salaam.

Shindano hilo ufanyika kila mwaka kwa lengo la kumuenzi mwasisi ya Klabu ya gofu ya Lugalo Jenerali Mstaafu George Waitara.

Akizungumza na wanahabari Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amesema shindano hili linawashirikisha wachezaji mbalimbali kutoka Klabu za mchezo huo hapa nchini.

Amezitaja klabu zitakazoshiriki kuwa ni Moshi club, Arusha Gymkhana, Mufindi club, Morogoro Gymkhana, Dar es Salaam Gymkhana, Sea Cliff Zanzibar, Kill Gofu pamoja na TPC Club.

Luwongo amesema shindano hilo litakuwa la siku moja ambalo litatanguliwa na la wachezaji wa kulipwa watakaocheza Januari 28.

Amesema shindano hili halitashirikisha watoto kutokana na aina ya mdhamini waliokuwa nae katika shindano hilo.

"Wanaoruhusiwa kushiriki ni wachezaji ridhaa kwa maana div A, B, C pamoja na Seniors na wanawake,"

Aidha Luwongo amesema mpaka sasa mwitikio umekuwa mkubwa kwa washiriki kujiandikisha ambapo wamefika 100 na zoezi linaendelea mpaka Alhamis.

"Kwa ambao bado hawajajiandikisha nafasi bado zipo nawaomba waendelee kujitokeza kwa wingi,"amesema Luwongo.

Amewashukuru wadhamini wakuu wa shindano hilo Serengeti Breweries kwa kujitoa kwao kudhamini shindano hilo.

Huku Nahodha wa Gofu Meja Japhet Masai amesema shindano hilo litakuwa la mashimo 18 ambapo washindi wa neti watapatikana.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz