Kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Hayati John Pombe Magufuli kimeonekana kuwagusa wachezaji wa gofu ambao wengi walionekana kuwa na mategemeo makubwa kuwa angeweza kuusimamia mchezo huo uzidi kukua hapa nchini na hata katika bara la Afrika. Katibu mkuu wa Chama cha Gofu cha Wanawake Tanzania, Madina Iddi Amesema wakati wa utawala wa rais Magufuli mchezo huo ulikuwa na mafanikio makubwa ikiwemo Tanzania kutwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati mwaka 2019 katika mashindano yaliyofanyika Uganda. Madina amesema "Pia katika mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika yaliyofanyika nchini Ghana mwaka 2018 Tanzani tuliweza kushika nafasi ya pili tukiwakilishwa na wachezaji wanne nikiwemo mimi,Hawa Wanyeche, Angel Eaton na Neema Olomi. Mchezaji huyo alisema wamesikitishwa na msiba huo kwani matamanio yao ya kukutana na rais Magufuli hayajaweza kufanikiwa baada ya mauti kumkuta. "Tulipanga tuonane naye baada ya kushika nafasi ya pili katika mashindnao ya kuwania ubingwa wa Afrika mwaka 2018 na hata tulipotwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na kati 2019 bado tulikuwa na ndoto hiyo ya kukutana naye ili kumueleza changamoto zetu. Alisema kifo cha rais Magufuli ni pengo kubwa sana kwani aliweza kuwasaidia kwenda kwenye mashindano ya Afrika kupitia kwa viongozi aliowachagua wakati huo wa TANAPA. “Kwa hili pia tunamshukuru sana kwani viongozi aliowateua kipindi kile mwaka 2018 walitusaidia sana kufanikisha safari yetu ya kwenda Ghana, "amesema Madina. Judith Ally ambaye ni mchezaji wa gofu wa timu ya wanawake ya klabu ya Dar es Salaam Gymkhana amesema kwa upande wake atamkumbuka rais Magufuli kutokana alivyokuwa na tabia ya kutobagua michezo. "Kwa kweli alikuwa anafuatilia michezo yote na hata ukiwa kiongozi ndani ya chama huwezi kumdanganya kitu ,"anasema Judith Naye Saidi Ally mchezaji wa gofu wa kulipwa, amesema wamepata pigo kubwa kutokana na jinsi rais Magufuli alivyokuwa mfuatiliaji wa vitu na kujua matatizo ya kila mchezo. "Itachukuwa mda mrefu kuziba pengo lake kwani ni rais aliyeonekana kuwa mfuatiliaji wa kila eneo inasikitisha tumempoteza kiongozi mahiri,” anasema Ally.