Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Wacheza Gofu 12 kuiwakilisha Tanzania "European Tour Challenge"

IMG 20220322 WA0032 Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania , Chriss Martin, akizungumza na waandishi wa habari

Wed, 23 Mar 2022 Chanzo: mtanzania.co.tz

Jumla ya wachezaji 152 wa gofu wa kulipwa kutoka Mataifa mbalimbali ikiwamo Watanzania 12 ,wanatarajiwa kuchuana katika shindano la gofu lililopewa jina la ‘ European Tour Challenge litakalofanyika Aprili 7-10, 2022 kwenye viwanja vya klabu ya Kilimanjaro Golf Estate, jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari Machi 22, 2022 katika klabu ya Gofu Lugalo, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania(TGU), Chriss Martin, amesema ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufanya shindano hilo kubwa .

Martin amesema lengo ni kukuza mchezo huo na utalii nchini, huku akiamini litakuwa na matokeo mazuri katika sekta hiyo kwa sababu lina manufaa makubwa.

“Tangu Tanzania tumepata Uhuru hii ni mara ya kwanza kufanya shindano hili. Hatutaishia hapa bali litakuwa ni endelevu na litafanyika kila mwaka mwezi Aprili.

“Hili shindano pia linajumuisha ile kampeni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ya Royal Tour kwa hiyo Golf imekuwa ni ‘product’ kubwa na nzuri kwenye mambo ya utalii, ” amesema Martin.

Amefafanua kuwa wanafanyia kwenye uwanja wa Kilimanjaro Golf Estate kwa sababu ndiyo umekizi viwango vya Kimataifa na maandalizi yanaendelea vizuri kwa kushirikiana na Serikali.

Kwa upande wake Katibu wa Mashindano wa TGU, Enock Magile, ameeleza kuwa vigezo vya washiriki ni wale wenye viwango vya juu, huku akisema Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kila moja inatoa wachezaji wawili.

Akizungumza kwa niaba ya wadhamini wa mashindano hayo, Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Lumuli Minga, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kushudia michuano hiyo.

Chanzo: mtanzania.co.tz