Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Tanzania yajipanga kutwaa ubingwa wa kombe gofu Afrika

Glof Gymkana Tanzania yajipanga kutwaa ubingwa wa kombe gofu Afrika

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Timu ya Tanzania ya mchezo wa gofu, wametamba kutwaa ubingwa wa mashindano ya gofu Afrika yanayotarajia kuanza Septemba 6  jijini  Dar-es-Salaam.

Mashindano hayo ya gofu yanayojulikana Kama 'All Africa Challenge Trophy' yatafanyika kwa siku tatu kuanzia Septemba 6 hadi 9 mwaka huu yakishirikisha zaidi ya wachezaji wanawake 300 kutoka nchi 24 za Afrika.

Kwa Tanzania, jumla ya wachezaji wanne watawakilisha nchi, akiwemo bingwa mtetezi wa kipengele Cha mtu Mmoja mmoja Madina Idd, akiwa na wenzake watatu Hawa Wanyeche, Neema Olomi, Angel Eaton waliofanikisha nchi kubeba taji la mshindi wa Pili msimu uliopita wa mashindano haya.

Akizungumzia mashindano hayo, katibu wa chama Cha gofu Cha wanawake (TLGU) Madini Idd alisema kuwa wanayo furaha kubwa mashindano haya kufanyikia nyumbani kwani inawapa nguvu ya kuhakikisha wanatumia uwanja wao vema kutwaa ubingwa.

"Tunakwenda kutwaa ubingwa mwaka huu unaoshikiliwa na mtetezi Afrika Kusini, ndio maana unaona tumeanza mazoezi ya kambi mapema, lakini pia kuongeza mda wa mazoezi na zaidi morali yetu iko juu Sana kusubiri siku ya mashindano"

Alisema kuwa mazoezi yao wanayafanya chini ya makocha wawili, Rajabu Idd na Jofrey Leverian katika uwanja wa gofu wa Dar gymkhana wakiwa timamu bila majeruhi.

Alisema kuwa hadi Sasa maandalizi kuelekea mashindano hayo yanaendelea huku wakitarajia kuanza kupokea wageni jumamosi hii.

"Changamoto kubwa bado tunahitaji wadhamini  wa kuhakikisha tunamudu gharama za kuwahudumia wachezaji wetu kutoka nchi zote Kama nchi wenyeji, hivyo tunaomba taasisi na mashirika washirikiane na sisi kuhakikisha tunatunza heshima ya uwenyeji huu"

Kwa upande wake kocha wa timu hiyo, Rajabu Idd alisema kuwa timu yake inaendelea vizuri ambapo wanatarajia kufanya vizuri kwa msimu huu.

"Watanzania wanaweza kututegemea kwa ubingwa wa mwaka huu, kwani mashindano kufanyika nyumbani inaongeza kujiamini ksa wachezaji wetu, lakini zaidi mazoezi waliyoyafanya tunaamini watafanya sawa sawa na matarajio yetu"

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz