Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Tanzania, Kenya jino kwa jino Gofu Afrika

Tzk Pic Tanzania, Kenya jino kwa jino Gofu Afrika

Thu, 8 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mchuano mkali kwenye mashindano ya Afrika ya Gofu kwa wanawake ya All Africa  Challenge Trophy 'AACT' umeonekana kwa wenyeji Tanzania ambayo inapewa presha na jirani zao Kenya.

Mashindano hayo ya siku tatu yatafikia tamati kesho kwenye viwanja vya klabu ya Gymkhana Dar es Salaam huku kwenye michezo ya raundi ya kwanza, nchi hizo zikimaliza kwa mikwaju sawa.

Katika mechi za raundi ya kwanza, Kenya na Tanzania zimefunga mikwaju 148 kila moja huku Tanzania ikiwa kinara kwenye msimamo kwa kuongoza baada ya kuongoza pia kwenye mikwaju ya mchezaji mmoja mmoja.

Nahodha Watanzania, Hawa Wanyenche ndiye kinara kwenye msimamo huo akifunga mikwaju 69 katika raundi hiyo, akimpiku mkwaju mmoja, Mkenya Neema Wafula aliyefunga mikwaju 70.

Bobbi Brown wa Afrika Kusini amekamata nafasi ya tatu kwenye msimamo akiwa na mikwaju 72.

Nyota Watanzania anayetetea ubingwa kwa mchezaji mmoja mmoja, Madina Iddi alifunga mikwaju 79 na Angel Eaton alifunga mikwaju  80 katika raundi hiyo ambayo imeshirikisha wachezaji zaidi ya 50 kutoka mataifa 21 Afrika.

Akizungumzia matokeo hayo, nahodha Watanzania, Hawa Wanyenche amesema yamekuwa mwanzo mzuri kwao kwenye harakati za kuwania ubingwa.

"Niko vizuri, timu yetu imekuwa na mwanzo mzuri katika mechi za raundi ya kwanza, bila shaka tutakuwa na muendelezo huo hadi kwenye mechi za mwisho kesho," amesema Wanyenche.

Mashindano hayo yaliyodhaminiwa na The Royal and Ancient Golf Club of St Andrews  'RNA '  na wadhamini wengine nchini yatafikia tamati kesho kwa bingwa kutangazwa uwanjani hapo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz