Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Siri ni tu! kutusua golf kimataifa

GOLF.jpeg Siri ni tu! kutusua golf kimataifa

Mon, 14 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo amevitaka vilabu vya Mchezo wa Gofu nchini kuenzi Uadilifu, Mila na taratibu za mchezo wa huo Ili kulinda vipaji na kuwaandaa vijana kushiriki mashindano ya kimataifa.

Luwongo ameyasema hayo wakati wa hafla ya ufungaji wa shindano la "Morogoro Open 2023" lililomalizika Jana Jumapili Mkoani Morogoro.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU) Girman Kasiga amesema haye yakizingatiwa yataongeza chachu katika ukuaji wa mchezo wa Gofu nchini.

Katika Shindano hilo mshindi wa kwanza ni Godfrey Leverian wa Morogoro Gymkhana aliyeshinda mikwaju ya (Gross149), huku wapili akiwa ni George Sembi wa TPC Mikwaju ya (Gross 152) na nafasi ya Tatu ikishikwa na Marius Kajuna wa Lugalo Mikwaju (Gross 158).

Shindano hilo limehitimishwa jana ambapo zaidi ya wachezaj 98 walishiriki shindani hilo kupitia vilabu vya Mufindi, Kilombero, TPC Moshi, Arusha, Kili Golf, Lugalo na wenyeji Morogoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live