Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Singo aongoza mamia ufunguzi gofu Afrika

Singo Pic Data Singo aongoza mamia ufunguzi gofu Afrika

Mon, 5 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Maendeleo ya michezo nchini, Yusuph Singo amewaongoza mamia ya wanamichezo katika ufunguzi wa mashindano ya Afrika ya Gofu kwa wanawake ya All Africa Challenge Trophy 'AACT' hii leo kwenye viwanja vya klabu ya Gymkhana, Dar es Salaam.

Wanamichezo wa mataifa 21 wamepandisha bendera za nchi zao na kupigiwa nyimbo za taifa uwanjani hapo kama ishara ya ufunguzi wa mashindano hayo ya siku tatu yatakayoanza kuchezwa kesho nchini.

Mbali na Singo, viongozi wengine wa gofu Afrika wakiongozwa na rais wa AACT, Monica Ntenga na viongozi wengine kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Tanzania yenye nyota wanne, Hawa Wanyenche, Madina Iddi, Neema Olomi na Angel Eaton ndiyo ilikuwa ya kwanza kupandisha bendera ya taifa wakifuatiwa na mataifa mengine.

Mataifa hayo ni Nigeria, Botswana, Malawi, Uganda, Togo, Rwanda, Zimbabwe, Afrika Kusini, Kenya, Namibia, Ghana, Burkina Faso, Morocco, Mali, Zambia, Ivory Coast, Mauritius, Misri, Sierra Leone, Cameroon na wenyeji Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mohammed Mchengerwa, Singo amesema, Tanzania imepata bahati ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Amesema mashindano hayo ni kama yalivyo ya Afcon kwenye soka, hivyo Tanzania imeweka historia kubwa kwenye gofu.

"Tunatarajia timu yetu itafanya vizuri, habari njema ni kwamba Tanzania ndiye bingwa mtetezi, hivyo sina wasiwasi na ubingwa," amesema.

Rais wa Chama cha Gofu wanawake Tanzania 'TLGU', Sophia Viggo amesema hamasa imekuwa kubwa licha ya Tanzania kuwa mwenyeji kwa mara ya kwanza.

"Naishukuru RNA 'The Royal and Ancient Golf Club of St Andrews kuwa mdhamini wetu mkuu na kufanikisha mashindano haya kwa kiwango bora.

Kocha wa timu ya Tanzania, Rajabu Iddi Pembe amesema vijana wake wako tayari kwa ushindani, wamekamilisha programu ya mazoezi na kinachosubiliwa ni matokeo tu ambayo yatajulikana Septemba 8.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live