Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Mzuka wa Gofu umepeleka elimu kwa jamii

Golf Mzuka Mzuka wa Gofu umepeleka elimu kwa jamii

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Rais wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Gilman Kasiga amesema Gazeti la Mwanaspoti kupitia Mzuka wa Gofu, limesaidia mchezo huo kueleweka haraka kwa jamii.

Kasiga ameyasema hayo leo kwenye viwanja vya Gofu vya Lugalo yanakoendelea mashindano ya NBC Waitara Trophy, 2024.

Kiongozi huyo alisema, Mwanaspoti limekuwa mdau mkubwa wa kuusapoti mchezo huo ambao awali haukujulikanika kama ilivyo sasa.

"Mwanaspoti kupitia Mzuka wa Gofu limefanya kazi kubwa sana, kwa sasa naona jamii inauelewa mchezo huo,mlichofanya ni kitu kikubwa sana, kama TGU tunakithamini na kuwapongeza," amesema Kasiga na kuongeza;

"Tunawaomba muendelee kuilimisha jamii, kwani mchezo huo una fursa nyingi,ajira na mazoezi."

Mzuka wa Gofu ni kurasa maalumu zinazozongumzia mchezo wa Gofu na hutokea kila Jumatatu ikiwa na habari mbalimbali na uchambuzi wa mchezo huo, ikiwa ni sehemu ya Mwanaspoti kutangaza michezo mingine nje ya soka.

Chanzo: Mwanaspoti