Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Mpo? Kiingilio gofu ni Sh 800,000 Marekani

Tiger Woods 6 Mpo? Kiingilio gofu ni Sh 800,000 Marekani

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati nyumbani Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa ni ngumu mtu kutoa hata laki moja kwa ajili ya kununua tiketi ya kuangalia mashindano ya gofu, kwa wenzetu ambako mchezo huo umeshika kasi mtu kutoa Sh800,000 kuangalia watu wanavyoonyeshana ufundi ni jambo la kawaida.

Kwa wadau na mashabiki wa mchezo huo duniani kwa sasa wanajiandaa na tamasha la Coors Light Birds Nest katika mashindano ya Phoenix Open 2024 ya Waste Management yatakayofanyika Ijumaa ya Februari 9, kwenye Uwanja wa TPC Scottsdale, Marekani wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 20,000.

Ni zaidi ya tukio kubwa kutokana na maandalizi ambayo yamefanywa huku wasanii wakubwa na maarufu nchini humo wakiwa sehemu ya tukio hilo kwa ajili ya kutumbuiza, kwa orodha ya awali atakuwepo rapa, Post Malone.

Pamoja na Tanzania na Ukanda wa Afrika Mashariki bado hazijafikia hatua ya watu kuhamasika kwenye gofu kwa kiwango kikubwa kama ilivyo mataifa yaliyoendelea, ila kaa ukijua huu sio mchezo wa kinyonge kwani kwenye tamasha hilo huko Marekani viingilio ni Dola 350 ambazo ni Sh 879,900.

Ukilipa kiwango hicho cha fedha unahudumiwa kibosi kwenye tamasha hilo ikiwemo kupata chakula na kinywaji cha kukupa vaibu la kushangilia mapigo ya gofu kutoka shimo moja kwenda lingine.

Kama ilivyo kwenye soka huku napo wapo mashabiki wa kweli wa mchezo huo na wanapata raha wanapoutazama mchezo huo, kama anavyoeleza mmoja wa mashabiki wakubwa wa mchezo huo Marekani.

“Niletee mashindano yoyote kuanzia ya kandanda yale ya Kombe la Dunia la FIFA, mchezo huu ni mzuri zaidi ya yote,” alisema Nicholas Bommarito, shabiki wa mchezo huo Marekani.

Miongoni mwa wachezaji maarufu wa mchezo huu ni Phil Mickelson ambaye alialikwa kwa mara ya kwanza kucheza mashindano hayo akiwa bado kwenye timu Jimbo la Arizona.

Mchezaji maarufu mwingine anayetamba duniani ni Tiger Woods na alionyesha ubora wake kwenye mashindano hayo yaliyofanyika kipindi kulipuibuka janga la Uviko-19. Mkali huyo ni mmoja wa mastaa wa mchezo huo aliyevutia wachezaji wengi baada ya kufanya vyema mwaka 1997.

Chanzo: Mwanaspoti