Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Gofu wanawake wapata viongozi wapya, Queen ashinda Urais

B507E66F CA6A 42B5 A844 4D540B9FBBB8.jpeg Gofu wanawake wapata viongozi wapya, Queen ashinda Urais

Sun, 26 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mmoja wa wachezaji gofu maarufu wa kike, Queen Siraki ameibuka mshindi wa kiti cha Urais wa Chama cha mchezo wa gofu cha wanawake nchini (TLGU) katika uchaguzi uliofanyika Jumamosi jioni kwenye klabu ya Lugalo.

Katika uchaguzi huo uliowashirikisha jumla ya wapiga kura 26 kutoka klabu mbalimbali, Queen alishinda kwa vishindo baada ya kupata kura zote 26 na kuchukua nafasi ya Sophia Viggo ambaye hakugombea. Siraki ambaye ni mfanyakazi wa benki ya Exim alisema kuwa amefurahi kushinda nafasi hiyo na kazi kubwa waliyokuwa nayo ni kuendeleza mchezo kwa ngazi zote, kuanzia ya chini mpaka kwa wakubwa.

“Nimefurahi kushinda kiti hiki na kazi yetu kubwa kwa sasa ni kuutangaza mchezo kwa wadau na kuendeleza kufikia hatua ya juu kabisa ya maendeleo. Kamati mpya ya utendaji imeundwa na viongozi wenye uchu wa maendeleo na naamini kwa ushirikiano, tutafikia malengo yetu,” alisema Siraki.

Mbali ya Siraki kuchaguliwa katika nafasi ya Rais, Ayne Magombe alishinda nafasi ya Makamu Rais kwa kupata kura 25 kati ya 26 huku nafasi ya katibu mkuu ikichukuliwa na Yasmin Chali aliyepata kura 24 kati ya 26 huku Joyce Ndyetabura akishinda nafasi ya mweka Hazina kwa kupata kura 25 kati ya 126 na Hawa Wanyeche akichaguliwa kuwa katibu wa mashindano kwa kupata kura 24 kati ya 26.

Kwa upande wake, Yasmin Chali alisema kuwa wana malengo makubwa sana ya kuendeleza mchezo huo hapa nchini na kuitangaza nchi nje ya mipaka yake kupitia mchezo huo.

“Tuna wachezaji wengi sana wenye vipaji ambao wana malengo ya kufikia hatua ya juu kabisa. Kazi yetu ni kuweka mipango ya maendeleo na kuwafanya wachezaji kuwa na furaha na pia kushiriki katika mashindano mengi zaidi, nchini na nje ya nchi pia,” alisema Yasmin.

Chanzo: Mwanaspoti