Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Gofu ukipiga hesabu vizuri wewe ni tajiri

Gksf Gofu ukipiga hesabu vizuri wewe ni tajiri

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bila hesabu kwenye gofu hutoboi, ipo hivi: Ili handcup zako ziwe ndogo, inatakiwa akili kubwa kwenye upigaji wa mipira kwenda shimoni.

Viwanja vya gofu vyenye ubora duniani vina levo par 72, mchezaji anaweza akapiga idadi hiyo ama pungufu, hao ni wenye handcup ndogo kwa lugha inayoeleweka wachezaji wenye uwezo mkubwa.

Japokuwa inaweza ikatokea hata wale wenye viwango bora (handcup) wakazidisha upigaji wa saizi ya kiwanja, ila wanaofanya makosa mengi ni wale ambao handcup zao ni nyingi.

Mzuka wa gofu kupitia gazeti la Mwanaspoti, linakuchambulia kwa njia ya data kwa nini gofu ni kama pacha na hesabu, hiyo ni kwa sababu ili handcup zako ziwe ndogo, hesabu yako lazima ziwe kali na za umakini kwenye upigaji.

GROSI NA NETI

Ukisikia neno grosi kwenye gofu ni alama anazohesabiwa mchezaji kutokana na mipira aliyopiga bila kupunguza handcup zake na saizi ya kiwanja (72).

Ikitokea kapiga 78 inakuwa ni hiyo hiyo na hiyo inatumika kwa mapro na wachezaji wa ridhaa wanaoanzia handcup 5- hadi + ambao wanaujua vizuri mchezo huo na wanaweza wakatamani kuingia kwenye upro. Kwa upande wa neti zinapatikana kutokana na mipira uliyopiga unatoa na handcup.

Mashindano yaliyomalizika hivi karibuni ya Lina PG Tour, kwenye Viwanja vya TPC Moshi Club, huku bingwa kwa upande wa Maproo akiwa ni Nuru Mollel matokeo kwenye ubao yalisomeka kapata -7.

Je, unataka kufahamu hiyo -7 ilipatikanaje? Mashindano hayo yalichezwa siku nne ambazo wamezidisha na levo par 72 ya kiwanja, ikapatikana 288 wametoa na 7, hivyo Mollel alipata grosi 281 kwa siku nne (72x4=288-7=281).

Matokeo ya awali Mollel alitoka sare na Fadhili Nkya hivyo wakaenda kurudiana kiwanja namba 18 ambapo Mollel alipiga mipigo mitatu mpira kwenda shimoni na Nkya alipiga minne, hivyo akamaliza nafasi ya pili kwa -7 hiyo hiyo akiwa nyuma kwa mpigo mmoja.

Mollel anayechezea klabu ya Arusha Gymkhana baada ya kushika namba moja alijinyakulia kitita cha Sh6.8 milioni kwa upande wa wachezaji wa ridhaa ni Ally Mcharo wa TPC Moshi aliyepata score (+5) akiondoka na Sh2.2 milioni.

Kwenye matokeo ya gofu, ukiona +5 maana yake siku nne za mashindano zilizidishwa na levo par 72 na kujumuishwa na +5, hivyo Mcharo alipata jumla ya grosi 293.

Mshindi wa pili kwa mapro ni Nkya wa Dar Gymkhana aliyepata sScore (-7) na kuondoka na Sh4.3 milioni, Abdallah Yusuph aliyepata (+8) Sh3.4 milioni, Frank Mwinuka (+10) Sh2.7 milioni, Hassan Kadio (+13) aliyepata Sh2.2 milioni, Isaac Wanyeche (+13) alijinyakulia Sh1.2 milioni, Rajab Idd (+17), John Said (+19), Salum Dilunga (+19) na Elisante Lembris aliyepata (+22) wote wakipewa laki 480,000.

Kwa upande wa wachezaji wa ridhaa mshindi wa pili ni George Sembi (+14) Sh1.3 milioni, Isiaka Daudi (+16) laki 900,000, Ibrahim Gabriel (+16) 700,000 na Elisha Fadhil (+18) aliyepata 570,000.

Zawadi ziko tofauti wakipendelewa zaidi mapro ambao wanazawadiwa kuanzia mshindi wa kwanza mpaka wa 10 huku wachezaji wa ridhaa wakipewa nafasi ya wachezaji watano.

Mapro wamepewa nafasi kubwa ya mashindano hayo kutokana na uchache wa mashindano ukitofautisha na wa ridhaa ambao wamekuwa wakishiriki mara kwa mara.

Mbali na hilo lengo kuu la Lina PG Tour ni kuwainua mapro na kuthamini mchango wao kwenye gofu kubwa zaidi ni kupewa nafasi ya kuwapeleka nje.

Mollel ambaye ni bingwa alikuwa na haya ya kusema: “PG Tour inatusaidia na kutujenga, ili tuweze kushiriki mashindano ya nje kama Uganda, Kenya, Rwanda na kwingineko, kwani awali ilikuwa ngumu, hatukuwa na mashindano ya hapa ndani.” Bingwa kwa mchezaji wa ridhaa ambaye ni Mcharo anasema: “Mashindano hayo ni afya nzuri kwa mapro wetu ambao hawana mashindano ya mara kwa mara, hivyo itawafanya wakacheze na ya nje ya nchi.”

Baada ya Moshi mashindano mengine ya awamu ya pili yanatarajiwa kufanyika mwezi ujao kuanzia Aprili 11-14 kwenye viwanja vya Sea Cliff Golf Resort & Spa visiwani Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live