Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

Gofu Afrika timu kuanza kuwasili nchini kesho

Afrika Pic Gofu Afrika timu kuanza kuwasili nchini kesho

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wakati timu kutoka mataifa 23 zikitarajiwa kuanza kuwasili nchini kesho Ijumaa tayari kwa mashindano ya gofu ya wanawake ya All Africa Challenge Trophy 'AACT' wenyeji Tanzania imeweka msimamo wa ubingwa.

Mashindano hayo yataanza Septemba 6 yakishirikisha nchi za mataifa 24 Afrika, Tanzania ikiwakilishwa na Hawa Wanyenche, Madina Iddi, Neema Olomi na Angel Eaton.

Kocha wa timu hiyo ijulikanayo kama 'Tanzania One Team' Rajabu Iddi Pembe ameeleza matarajio ya ubingwa ya mashindano hayo.

Rajabu amebainisha hayo leo wakati wa kuitambulisha timu ya taifa katika hafla iliyoongozwa na  kaptein wa Gofu wanawake wa klabu ya Gymkhana, Merian Mugo na rais wa Chama cha Gofu cha wanawake Tanzania, (TLGU), Sophia Viggo kwenye viwanja vya Gymkhana.

Alisema wamejiandaa ipasavyo  kulipigania taifa ili kubakisha nchini ubingwa wa mashindano hayo yaliyodhaminiwa na kampuni za Serengeti Breweries Limited (SBL), Great Lakes, Pepsi, Oryx, Prima Afro, National Internet Data Centre (NIDC),  Garda World, Mohamed Enterprises Tanzania Limited (METL), Wadsworth, Freight & Transport, Capital Finance Ltd, Cornerstone Solutions Ltd, Savvy Fm, Liquid, Toyota Tanzania, benki ya CRDB na Simba VIT.

Amesema wamefanya maandalizi ya kutosha na sasa wako katika hatua za mwisho mwisho, akisisitiza kwamba wamebakisha 'shot' ndogo ndogo kukamilisha programu yao ya mazoezi.

Sophia Viggo,  rais wa TLGU amesema timu kutoka nje ya nchi zitaanza kuwasili kesho na  Septemba 4 na 5 zitafanya mazoezi ili kuzoea viwanja

Nchi hizo ni Nigeria, Botswana, Malawi, Uganda, Togo, Rwanda, Zimbabwe, Afrika Kusini, Kenya, Namibia, Senegal, Ghana, Burkina Faso, Morocco, Tunisia, Mali,  Zambia, Ivory Coast, Mauritius, Gabon, Misri, Sierra Leone na Cameroon.

Aidha Viggo amewaomba wadau zaidi kujitokeza kuendelea kuwasapoti akibainisha kwamba timu ya taifa inahitaji jezi, vifaa, lakini pia usafiri na malazi kwa timu zote shiriki.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz