Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Golf

120 kuliamsha Lugalo Open 2024

Golf Lugalo 120 kuliamsha Lugalo Open 2024

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wachezaji zaidi ya 120 wa gofu wanatarajia kushiriki katika mashindano ya wazi ya ‘Vodacom Lugalo Open 2024’.

Mashindano hayo, yalioandaliwa na klabu ya Lugalo yatafanyika kwenye viwanja vya klabu hiyo kati ya Julai 5-7.

Mwenyekiti wa klabu ya Lugalo, Brigedia Jenerali Mstaafu, Michael Luwongo aliliambia Mwanaspoti, klabu zote za hapa nchini zimealikwa pamoja na wachezaji kutoka nchi jirani.

Alitaja klabu zilizotumiwa mwaliko na anaamini zitashiriki ni; Mufindi, Morogoro Gymkhana, Kili Golf, TPC, Moshi Gymkhana, Dar es Salaam Gymkhana, Morogoro Gymkhana, Arusha Gymkhana, Kilombero na wenyeji Lugalo.

Alisema katika mashindano hayo wachezaji watashindana kwa mfumo wa ‘Stroke Play’, huku Mkurugenzi wa Masoko kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo yaani Vodacom, Allen Meena, alisema kwa nafasi waliyopewa ya udhamini ameahidi utakuwa ni ushirikiano endelevu.

Mwenyekiti wa Chama cha Gofu nchini (TGU), Girman Kasiga alitoa wito kwa wachezaji wote watakaoshiriki shindano hilo washindane kwa juhudi kubwa.

“Katika shindano hili washindi watapata nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa,” alisema Kasiga.

Chanzo: Mwanaspoti