Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wenye madaraka, mali wanatakiwa kuyatumia kwa hofu ya Mungu

Wenye madaraka, mali wanatakiwa kuyatumia kwa hofu ya Mungu

Fri, 27 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti.  Watu wenye uwezo wa mali na madaraka wanatakiwa kuzitumia kwa manufaa ya wengine ili kutimiza mapenzi ya Mungu.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Desemba 25, 2019 na Padri wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Mugumu Jimbo Katoliki la Musoma nchini Tanzania, Joel Marwa katika misa ya Krismasi Padri huyo amesema kwa kufanya hivyo, kunadhihirisha mapenzi mema kwa wanadamu.

“Yesu alizaliwa zizini eneo chafu, lakini leo dunia inamwabudu kama mkombozi, alidharauliwa na watu wenye fedha na vyeo lakini leo wanapiga magoti kumwabudu, sasa mimi na wewe tunajiinuaje kwa vyeo na mali tulizonazo ambazo tutaziacha, lazima tutambue yote tuliyonayo tunatakiwa yafanyike kwa kufaidiana,” amesema.

 

Amesema Herode alikuwa na nguvu lakini alishindwa kuzima nguvu ya Yesu kwa kuwa ni mpango wa Mungu, hivyo wenye nguvu, fedha wanatakiwa kuwahudumia wenzao wanyonge badala ya kuwakandamiza.

“Kuna watu leo watakunywa na kula na kulewa huku jirani zao hawana chakula, hiyo si maana halisi ya kuzaliwa kwa Yesu,” amesema.

Amesisitiza upendo aliosema ni msingi mkuu wa Mungu kwa wanadamu na kwamba, watu waache ubinafsi ambao unaanza kuwatenganisha ndugu kwa ndugu.

 

Columnist: mwananchi.co.tz