Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wazazi wenye watoto waliofanikiwa wana tabia hizi

Mon, 15 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mzazi yeyote mwema hupenda watoto wake wasiingie kwenye matatizo, wafanye vizuri masomoni na kazi za maana utu uzimani. Kwa kuwa hakuna muongozo maalumu wa kukuza watoto wenye mafanikio, saikolojia imeweka bayana sababu lukuki za kumtabiria mtoto mafanikio na si ajabu nyingi ya sababu hizo hutokana na wazazi.

Yafuatayo ni mambo ya kufanana kwa wazazi wenye watoto waliofanikiwa.

Huwafanya watoto wajishughulishe

“Kama mtoto haoshi vyombo, hafui nguo zake wala kufanya usafi ndani ya nyumba ina maana kuna anayefanya kwa niaba yake” anasema Julie Lythcott-Haims, mtaalamu wa malezi. Watoto wanaojishughulisha katika kazi hizi si tu wanafahamu kuhusu kazi, pia wanajifunza kuwa kila mtu anatakiwa kuwajibika ili kuchangia maendeleo ya familia, jamii na hata taifa.”

Huwafundisha watoto stadi za jamii

Watafiti wa vyuo vikuu vya Marekani wameona uhusiano mkubwa kati ya stadi za maisha walizozipata watoto wakiwa elimu ya awali/msingi na mafanikio yao kama watu wazima baada ya miongo miwili. Imebainika watoto wenye kujiamini, kushiriki kazi za jamii, wenye stadi za maisha na kushirikiana vizuri na wenzao bila msukumo na wenye kuweza kutatua matatizo na kuwa msaada kwa wengine wana nafasi kubwa kufikia malengo ya elimu ya juu na kupata kazi/ajira ukilinganisha na wale ambao hawakufunzwa stadi za maisha katika umri mdogo.

Wanayo matarajio makubwa

Tafiti zinaonyesha, matarajio ya wazazi juu ya watoto wao yana mchango mkubwa kwa mafanikio ya watoto, hii ni kwa sababu wazazi hushiriki kikamilifu kuhakikisha wanawaongoza watoto kufikia malengo. Wazazi wenye maono ya elimu ya juu kwa watoto wao huhakikisha wanaweka jitihada kuwasaidia kufikia ndoto hiyo bila kujali kipato wala miliki walizonazo.

Wana mahusiano mazuri baina yao – ni viongozi na si watawala

Watoto waishio kwenye familia zenye migogoro, iwe wazazi wamepeana talaka au wako pamoja, nk. huwa na matatizo ya kisaikolojia yanayopelekea kukosa maarifa ya kushirikiana vyema na wenzao katika nyanja mbalimbali ukilinganisha na wale wanaoishi kaitika familia zenye upendo, amani na ushirikiano baina yao.

Wazazi hawa huwa na malengo endelevu kwa watoto wao na kufanya jitihada kuwekeza muda wao mwingi katika kutoa muongozo na kufuatilia muenendo wa maisha ya watoto wao. Mtoto hukua akijua kuna uongozi lakini wenye kumpa nafasi ya kukosea kama binadamu na kupatiwa fursa ya kujifunza kutokana na makosa na matokeo ya maamuzi yao

Tano. Wazazi wao wamepata elimu ya juu na/au wanayo hali nzuri kiuchumi.

Tafiti zinaonyesha kwamba wanawake waliohitimu elimu ya juu wana uwezekano mkubwa wa kukuza watoto wenye kufikia kiwango hicho cha elimu na zaidi.

Utafiti unaendelea kuonyesha kuwa kiwango cha elimu cha mzazi wa mtoto kinachagiza uwezekano wa mtoto kupata maendeleo katika nyaja lukuki maishani hususani masomoni.



Columnist: mwananchi.co.tz