Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wananchi mjadala wa Jukwaa la Fikra watakiwa kujikita kwenye mapendekezo yenye tija

20882 JUKWAA+PIC TanzaniaWeb

Sat, 6 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL),  Francis Nanai amewataka wananchi wanaoshirikia mjadala wa Jukwaa la Fikra kujikita katika mapendekezo yenye tija.

Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 4, 2018 wakati akimkaribisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kufungua rasmi mjadala wa pili wa Jukwaa la Fikra la Mwananchi wenye kauli mbiu ‘Kuelekea Uchumi wa Viwanda’, Nanai amesema ni wakati mwafaka kwa mawazo mtambuka kujengwa ili kusaidia watunga sera.

“Leo tunazungumzia ajenda ya uchumi wa viwanda ni kipaumbele cha Serikali ya awamu ya tano, nashauri Watanzania wote kutumia jukwaa hili la fikra kuzungumza kwa umakini na tujikite kutoa mapendekezo yenye tija,” amesema Nanai na kuongeza:

 

“Kwa mustakabali wa nchi yetu ili tukitoka hapa watunga sera waweze kupata kitu cha kwenda kukifanyia kazi.”

 

Amesema mjadala wa kwanza ulioandaliwa na MCL ulizungumzia sekta ya afya, mada ikiwa ni magonjwa yasiyoambukiza (NCDs).

Columnist: mwananchi.co.tz