Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Walichokisema wananchi majibu ya Membe kwa Rostam

58359 Pic+membe

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Siku moja baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe kumtaka mfanyabiashara maarufu, Rostam Aziz kuacha kuzungumzia watu badala yake ajikite kuzungumzia “mambo makubwa ya nchi”, wananchi wametumia mitandao mbalimbali ya kijamii kuzungumzia ‘vita’ ya maneno ya wawili hao.

Membe alitoa kauli hiyo jana Ijumaa Mei 17, 2019 akijibu swali kuhusu ushauri uliotolewa na Rostam kwake kwamba asichukue fomu za kuomba kupitishwa na CCM kuwania urais mwaka 2020 kama ilivyo utamaduni wa chama hicho tawala.

Rostam alitoa ushauri huo katika mahojiano na Mwananchi yaliyofanyika Desemba 2018, lakini sehemu ya video hiyo kurushwa hewani tena kwenye mitandao ya kijamii kuanzia katikati ya wiki hii.

Katika ukurasa wake wa Twitter aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS), Fatma Karume  ameandika kuwa Rostam ametumwa kwa Dual purpose (makusudio mawili); kwamba moja ni kumhakikishia Membe na pili ni kutukumbusha kuwa uchaguzi mwaka 2020 Magufuli (Rais John) hauepukiki.

“Tusijaribu kukariri tunaweza kutumia haki yetu ya kura kumuondoa maana CCM imeshaamua urais 2020 ni haki ya Magu. Kusema kweli kwa jibu hili nimemuheshimu sana Membe,”

Jimmy James aliweka picha ya Membe katika ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter ameandika, “hapo umenena kama mzee mwenye busara,”.

Habari zinazohusiana na hii

Mwingine, J Kalike aliweka andiko lake lilionyesha kusifia uamuzi wa Membe na kusema, “Mkiwa 20 kama nyie mambo yatanyooka maana huo ndiyo uzee mwema,”.

“Kuna tetemeko kali hivi karibuni kaeni tayari,” ameandika Jovin Philipo.

 

Columnist: mwananchi.co.tz