Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wajane : Tunasingiziwa tumeua wame zetu

Sun, 24 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Wajane Tanzania (Tawia) kimesema changamoto kubwa inayowakumba wajane hapa nchini ni kukosa urithi wa ardhi na mali ambazo wamechuma na wenzao wao wakati wa uhai.

Hayo yamebainishwa leo Juni 23 na Mwenyekiti wa Bodi ya chama hicho Martina Kabasina katika maadhimisho ya Siku ya Wajane duniani ambayo katika kanda ya Pwani yamefanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini hapa na kitaifa yamefanyika Wilayani Loliondo.

Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi Kabasina amesema kuna matukio mengi ya wajane kufukuzwa katika nyumba zao lakini pia kusingiziwa kuwaua waume zao ili iwe sababu ya kuwanyanyasa.

"Tunakuomba mgeni rasimi Serikali ijitahidi kutokomeza vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wajane kwani hata haki zao ambazo zipo kisheria mchakato wake wa kuzipata umegubikwa na rushwa. Tusaidiane kumaliza unyanyasaji kwa wajane na kuwaondolea vizuizi vyao vya kiuchumi," amesema Kabasina.

Amesema hata wagane (wanaume waliofaiwa na wake)wanachangamoto kama wajane lakini wajane ziko tofauti na athari zake zinawagusa mpaka watoto kwani hujikuta wakikosa elimu na wengine hukumbwa na unyanyasaji wa kingono.

Hata hivyo amesema Tawia inahitaji eneo la ekari tano kwaajili ya ujenzi wa kijiji cha wajane (eneo maalumu kwa ajili kushughulikia changamoto za wajane) na ekari 50 kwa ajili ya eneo la kiuchumi ambapo wajasiliamali wajane watakiwa wakufanyia shughuli zao za kibiashara.

Akijibu risala hiyo Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke Dk Sost Mosha amesema ni muhimu kwa wajane kujiunga katika vikundi ili waweze kukopesheka na kujiinua kiuchumi.

 

Columnist: mwananchi.co.tz