Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Wachezaji kuweni basi na mshawasha wa kucheza soka nje

10367 Ibra+Bakari TanzaniaWeb

Mon, 6 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

T angu Ligi Kuu Bara kumalizika na Kombe la Shirikisho ambalo Mtibwa ndiyo imetwaa ubingwa, nilichokiona hapa ni pilikapilika za klabu za Ligi Kuu kuwania usajili wa wachezaji kwa msimu ujao.

Sawa, hicho kilikuwa kipindi mchezaji alitakiwa kujiwahi, mchezaji kukomaa kuhakikisha kuwa anapata timu kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu, kwani ikimalizika hapa, ndiyo basi tena.

Unajua, kumalizika kwa Ligi Kuu ni kama maji yamemwagika Jangwani, kila mmoja anayawahi kwa ajili ya kutii kiu yake. Nimechukulia mfano huo, kwa kuwa harakati zimekuwa kubwa kupitiliza.

Na harakati zimekuwa hivyo kwa kuwa kuna wachezaji ambao mikataba yao ilimalizika, kuna wachezaji walioachwa, kuna waliotaka kuondoka japo klabu iliwahitaji na kuna wale ambao wawepo sawa na lolote kwao sawa. Kipindi hicho ndiyo kile cha mavuno kwa waliokuwa wanajituma na kuonyesha kiwango. Ndiyo hapa unasema kuwa kuwa mchezaji anabebwa na kiwango chake.

Klabu haiwezi kusajili mchezaji mchovumchovu akataka awekewe Sh50milioni mezani, kama mchezaji alikuwa anaendekeza starehe, ataishia signing on fees ya Sh5mil au hata chini ya hapo. Ndio.

Ninachotaka kusema, pamoja na kuwania kucheza katika klabu mbalimbali kubwa na zile za kawaida, bado nasema wachezaji wa Tanzania kuangalia soka nje ya mipaka. Wachezaji wamekuwa na mtazamo wa ndani ya boksi kuwa ninyi ni Ligi Kuu na Ligi Kuu ni ninyi. Hilo hapana.

Hata hapo Kenya, wachezaji wanajaribu. Wanahangaika kusaka mawakala na si kusubiri neeme ikudondokee, ukihangaika na Mungu atakusaidia kama mchezaji.

Kama mchezaji ni mkali, utakubalika tu kama ilivyo Kenya kwa sasa wamejaa Waganda, Wanyarwanda wako huko na katika viwango vya Fifa, wako juu.

Zambia wako juu kisoka,

Ilikuwa nafasi ya kumsumbua aliyekuwa kocha wa Yanga, George Lwandamina kuwaunganisha kupata timu halafu mchezaji mwenyewe anaendelea ikiwemo kuwatafutia mawakala, lakini ajabu wachezaji wetu wanazitolea macho; Simba, Yanga, Azam au Mtibwa. Lwandamina anainoa Zesco kwa sasa.

Kuchangamka na kwenda kucheza nje, kuna faida mbili kubwa; Mosi, kwa timu ya taifa, itakuwa na wachezaji wengi wenye chgangamoto mbalimbali na hata inapokuja suala la timu ya taifa, wanakuwa wameiva kupitia ligi mbalimbali za nje.

Kama mchezaji anacheza nje, changamoto anazopata hawezi kuwahofia tena Ghana, Nigeria, Ivory Coast, Algeria au Senegal. Inapendeza, Inaundwa Taifa Stars yote inayocheza nje na waliopo nyumbani wanagombania namba ya CHAN wenyewe.

Siku hizi hata Uganda na Kenya sehemu kubwa wanatumia mapro wao tu kwenye timu ya taifa.

Pili; kucheza nje, mchezaji anaongeza kipato. Kucheza nje ni pesa, wachezaji wanashindwa tu kuelewa. Kama mchezaji ni kijana, unauweza, nini cha kuhofia? Anza madaraja ya chini, utapanda tu taratibu lakini ukifuata misingi ya soka.

Uzuri wa soka haichezwi chumbani kwamba utajificha, ni hadharani mbele ya kadamnasi ya mashabiki.

Kuwa na mawazo ya kucheza nje peke yake ni pesa kwa hiyo siamini kama mchezaji atakaa na kukomalia kuzitaka Simba, Yanga, Azam au Mtibwa na nyingine. Wachezaji wanatakiwa kufikiri nje ya boksi kila mara.

Columnist: mwananchi.co.tz