Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Waajiri wanaowahenyesha wajawazito wanyoshewa kidole

11770 WAJILI+PIC TanzaniaWeb

Thu, 19 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Serikali imesema tabia za baadhi ya waajiri kumpangia kazi ngumu mjamzito au mama anayenyonyesha ni ukwamishaji wa unyonyeshaji wa maziwa ya mama.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Julai 19, 2018 na kaimu mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya chakula na lishe Tanzania, Dk Vincent Assey katika semina kwa vyombo vya habari kuhusu wiki ya unyonyeshaji inayoanza Agosti Mosi hadi 7, 2018.

Amesema kulingana na takwimu, kuna ushahidi mkubwa wa faida za unyonyeshaji kwa mama na kwa mtoto.

Amesema kwa kutambua ukweli huo, Serikali ya Tanzania imechukua hatua mbalimbali kulinda, kuimarisha na kuendeleza unyonyeshaji.

“Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 inatambua unyonyeshaji ni haki ya mtoto na hivyo hutoa mafao mbalimbali ya uzazi ili kuwawezesha wanawake kumlea mtoto hususan kumnyonyesha ipasavyo,” amesema Dk Assey.

Amesema mwajiri haruhusiwi kumpangia mama mjamzito kazi ngumu na  hatari wakati wa usiku au unyanyasaji wa aina yoyote kwani kufanya hivyo kutasababisha kupungua kwa kingamwili za watoto, utapiamlo na kupunguza uhakika wa chakula hasa kwa watoto wachanga.

“Changamoto iliyopo katika suala hili ni wanawake wengi kufanya kazi katika sekta isiyokuwa rasmi, kazi binafsi na Kilimo,” amesema.

Ofisa mtafiti mwandamizi elimu na mafunzo ya lishe kutoka TFNC, Neema Joshua amesema maziwa ya mwanzo ya mama yana kinga mwili na chembechembe za vitamin A , yanasaidia mfumo wa chakula kwa mtoto ukomae na kulainisha tumbo na hata kuzuia manjano.

Takwimu za TDHS  mwaka 2015/16 zinaonyesha kuwa idadi ya watoto waliodumaa ni milioni 2,700,000, uzito pungufu 340,000 na ukondefu 160,000.

 

Columnist: mwananchi.co.tz