Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Vita ya Steve Nyerere na Mwana FA itaisha hivi

Tivu Vita ya Steve Nyerere na Mwana FA itaisha hivi

Fri, 25 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NAWAZA kwa sauti! Wakati msanii wa Bongo Fleva, MwanaFA anaingia kwenye vita ya maneno na mchekeshaji Steve Nyerere alisoma alama za nyakati?

MwanaFA, aliwaza kwa kina kama uamuazi wake ungemvunjia heshima kwa kuitwa ”pua” na kutiliwa shaka hata kwenye ushindi wa Ubunge wake wa Jimbo la Mheza, mkoani Tanga?

Kama aliwaza, thamani ya nafasi ya ubunge na kuunga mkono harakati za kutaka kumng’oa madarakani Steve Nyerere kwenye cheo chake cha msemaji mpya wa Shirikisho la Muziki Tanzania, ipi kubwa?

Nawaza; FA amefanya aliyofanya, kajibiwa alivyojibiwa na anashambuliwa kila kona kuna chochote cha maana amepata?

Nafikiri MwanaFA hakutazama alama za nyakati, angelijua ya gizani asingeingiza mkono na kujeruhiwa.

Ukiniuliza nini kifanyike kati ya kambi ya MwanaFA na Steve Nyerere baada ya yote haya kutokea; nitakujibu: “Kusameheana.” Ndiyo njia pekee ya kumaliza vita na mvutano wao.

Yawezekana MwanaFA kuna mahali alikosea; lakini bado makosa yake hayamuondolei sifa ya kuwa msanii mkubwa nchini na sasa ni mheshimiwa mbunge.

Hata kwa Steve Nyerere ambaye mara kadhaa amekuwa “akililia ukubwa” kuna shida naiona kwake; maana huwezi kuwa kiongozi wa watu wanaokuunga mkono tu na kuwatenga wanaokupinga.

Kama wewe ni msemaji wa shirikisho basi utakuwa msemaji wa wanamuziki wote; huwezi kusemea mafanikio halafu ukasema yakija hayo mafanikio yawatenge wanamuiki fulani walionipinga haiwezekani.

Nashauri, kwa kuwa shirikisho la wanamuziki wa Bongo lina safari ndefu liinahitaji zaidi umoja, kilichowafikisha hapo walipo ni utengano; wakiendelea kutengana watakufa mara mbili ya walivyokufa.

Mapato na umaarufu wa mwanamuziki utabaki kwenye ubora wa kazi yake haya mambo ya kuchonganisha mbwa mawindoni hayawezi kumfanya sungura akakamatika kirahisi.

@Stevenyerere2 unalo la kumwambia ndugu yako @mwanafa “Nisamehe” ili maisha yaendelee naye pia nacho cha kukuambia kama rafiki kuwa “Nisamehe” kwani ujenzi wenu ni wa nyumba moja hivyo hamtakiwi kugombea fito naamini hata serikali na waziri wa Utamaduni @mmchengerwa, @basata.tanzania mtakuwa mmesikia ushauri wangu.

Columnist: www.tanzaniaweb.live