Dar es Salaam. Viongozi mbalimbali wamefanya dua katika kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume katika kumbukumbu ya miaka 48 ya kifo chake.
Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein; Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume ni kati ya waliohudhuria dua hiyo.
Dua hilo limesomwa leo Jumanne Aprili 7, 2020 katika kaburi la kiongozi huyo.
Abeid Amani Karume alizaliwa Agosti 4, 1905 na kufariki Aprili 7, 1972 katika kitongoji cha Pongwe Wilaya ya Magharibi A, Kisiwani Zanzibar.
Mwanaye, Balozi Ali Abeid Karume amesema baba yake alikubali muungano kwa sababu alijua Afrika ni kitu kimoja.
“Asingekuwa Abeid Amani Karume huu muungano wetu Tanzania usingekuwepo na huo ndio ukweli wenyewe kwa sababu hii nchi ilikuwa inatawaliwa na Sultani.”
Pia Soma
- Mamia wajitokeza kuwania maeneo ya biashara Dodoma
- CAG abaini watumishi hewa
- Meneja wa Diamond asimulia alivyopona ugonjwa wa corona