Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Usiruhusu hali ya kubakwa na mumeo ikutokee

Mon, 16 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nimekuwa nikipokea malalamiko ya wanaume wakidai kila siku wanawabaka wake zao.

Unaweza ukashangaa kusikia mume anambaka mke wake. Usishangae wanabakwa na siyo mara moja wala mbili kwa mujibu wa wanaume wenyewe.

Ushuhuda huu pia nimeupata kwa wanawake kadha wa kadha baada ya kuwaelewesha maana ya wanandoa kubakana.

Maana yake ni pale mwanamume anapokuwa na hamu ya kukutana na mkewe halafu mke hana hamu wala mpango huo na akang’ang’ania msimamo wake bila kujali yeye ndiyo tiba ya mumewe.

Mwanaume kutokana na tamaduni za karne na karne ni mtu asiyekubali kushindwa hulazimisha kukutana na mkewe, hapo ndipo ubakaji unapoanzia.

Mwanamke atahusika, lakini hatashiriki kikamilifu huku akijitahidi mumewe ajue kuwa yeye hashiriki ama kwa kulia, kununa au kukaa mikao isiyo rasmi ambayo itampa shida anayelazimisha kutimiza azma yake kiasi cha kutumia nguvu au ukali.

Ikumbukwe kuwa tendo la ndoa linahitaji maandalizi na viungo vyake ili kulinogesha, ukilifanya kwa kulazimishwa ni baya na utazidi kulichukia.

Hivyo wakati wa kushiriki kila mmoja anapaswa kucheza katika nafasi yake kuhakikisha ushindi wa kishindo unapatikana.

Kumbuka sababu kuu ya kuoana bila kuzunguka na kumung’unya maneno ni hiyo, kupika, kufua, kupata watoto, kutunza nyumba ni mengineyo, lakini alikuoa ili apate raha na ajiachie katika tendo la ndoa unapombania anakuwa hakuelewi.

Kama kuna jambo linalofanya kazi chini kwa chini na kuharibu ndoa nyingi bila wahusika kujua ni mwanamke kumnyima mumeo haki ya tendo la ndoa.

Kuna neno moja wanawake wengi wanapenda kulitumia tena wakidhani ni sifa eti! sina hamu ya tendo la ndoa. Halafu yumo ndani ya ndoa ya watu wawili anazungumza akitumia nafsi moja hii inaonyesha namna wengi walivyo wabinafsi.

Unachotakiwa kufanya ni kupambana kurudi katika hali ya kawaida, na ninataka niwaambie wanawake walio ndani ya ndoa hii hali siyo sifa, hakikisha unaificha kama unayo kwa kushiriki kwenye hilo tendo kama inavyotakiwa.

Wanaume wakiwa na hali hiyo hupambana kwa kila njia ili wawe sawa, lakini wanawake sijui wamepatwa na nini hadi kuona kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa ni sifa na wanastahili kuwa nayo tena baadhi yao wanaiweka mbele kama tai.

Nasisitiza huu ni ugonjwa tena wa aibu kuwa nao mwanandoa, kama mnaufuga kwa makusudi jihadharini maana mtakuwa wagonjwa kamili na hakuna mwanaume aliyeoa anataka kupata shida wakati wa kujamiana kwa kumbaka mkewe kila siku.

Jambo hili ni hatari kwa mahusiano, licha ya kuwapo wanawake wengi wanaomendea wanaume waliooa kama fisi na mfupa, lakini inaleta picha mbaya mwanaume anaweza kufikiri mambo mengi kukuhusu.

Anaweza kufikiri hakuridhishi na umepata mtu anayekuridhisha, una wanaume wengi ndiyo maana ukifika wakati wake kujiachia unakuwa umechoka. Hatari mwanandoa kuruhusu mmoja kati yao kuwa na mawazo mabaya dhidi yake.

Inawezekana kama binadamu kuna siku huna hamu ya tendo la ndoa na kwa wanawake hili ni tatizo, lakini bado haikupi haki ya kumkatalia mumeo hadi atumie nguvu.

Narudia, tena nasisitiza ni aibu kwa mwanamke aliyeolewa kumkatalia mumewe tendo la ndoa hadi anabakwa. Shiriki tendo hilo muhimu kama inavyopaswa hata kama huna hamu jihamasishe na mshirikishe mwenza wako kurudi katika hali ya kawaida.

Columnist: mwananchi.co.tz