Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Unataka kumiliki gari kwa muda mrefu, Epuka makosa haya

84247 Gari+pic Unataka kumiliki gari kwa muda mrefu, Epuka makosa haya

Fri, 15 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Gari ni chombo cha usafiri amba-cho hutumiwa na watu kwa shu-ghuli mbalimbali. Gari linapoanza kutumika unakuwa mwanzo wa kupungua kwa thamani yake kul-ingana na matumizi ya dereva.Lakini habari njema ni kuwa unaweza kuliokoa gari lako na kulifanya lidumu muda mrefu kwa kuepuka baadhi ya tabia zisizo sahihi zinazoweza kuliua gari mapema.

Tahadhari hiyo itasaidia kuon-geza thamani ya gari lako, pia kuokoa fedha za matengenezo, kuliweka salama na kuepuka kusi-mama mara kwa mara pembeni ya barabara ili kubaini tatizo. Epuka makosa yafuatayo ili thamani ya gari idumu muda mrefu.

Kupuuzia taa za tahadhari

Taa za tahadhari ambazo zinaonekana mbele ya kioo sio mapambo, kila taa ina maana, usiipuuze. Mfano taa ya injini inaweza kuashiria jambo lisilo la kawaida kwenye mfuniko wa gesi, breki au mfumo wa upepo kwenye matairi.

Ikiwa taa hizo zitakuonyesha jambo lisilo la kawaida kwenye mfumo wa gari lako ni vizuri kuangalia changamoto iliyotokea na kuirekebisha mara moja kabla tatizo halijawa kubwa.

Umakini ukipita kwenye mashimo

Miundombinu ya barabara nyingi za Tanzania siyo rafiki kwa magari, umakini unahitajika hasa kwenye barabara zenye mashimo na ikiwezekana jitahidi kuyakwe-pa ili kulinda tairi za gari lako.

Mashimo yanapindisha magu-rudumu, kuliondoa gari kwenye muelekeo sahihi na kuharibu sehemu muhimu za breki.

Kutobadilisha mafuta mara kwa mara

Injini ya gari haiwezi kuwa na ufanisi ikiwa mafuta hayabadilishwi kwa wakati, ni muhimu kuangalia kama kuna mafuta ya kutosha kulainisha injini kulingana na mwongozo wa gari husika. Kuto-badilisha mafuta na kuchunguza mirija inayopeleka mafuta kwenye injini kunaiweka katika hatari ya kuharibika mapema. Pia, inahusisha mafuta yote yanayolainisha sehemu mbalimbali za gari.

Kupuuzia marekebisho madogo madogo

Marekebisho ya gari yana gharama lakini yasipofanyikwa kwa wakati yanaweza kuongeza gharama kubwa ikiwa kifaa fulani kimeharibika sana. Mfano kuche-lewa kubadilisha mpira unaozuia breki isichakae kunaweza kuon-geza gharama kubwa za kununua breki mpya. Kutobadilisha taa kubwa ya mbele kunaweza kusa-babisha ajali wakati wa usiku iki-wa taa imeharibika bila kutarajia.

Kutoangalia upepo kwenye matairi ya gari

Katika mambo ambayo yanasa-babisha upepo wa matairi kuisha mapema ni kutoweka kiwango cha kutosha cha upepo kwenye matairi. Hali hii inaweza kuathiri bajeti ya mafuta na usimamizi wa gari. Ni muhimu kuangalia kama kuna upepo wa kutosha kwenye matairi na inapaswa kuwa sehemu ya huduma za matengenezo.

Kutokuchunguza matairi ya gari

Wakati wa kuangalia kiasi cha upepo kwenye matairi unaweza kutumika pia kuangalia usalama wa magurudumu kama yamefung-wa vizuri, au kupasuka. Peleka gari kwa fundi ili kuondoa misumari au miiba kwenye matairi kabla tairi halijapasuka katikati ya barabara.

Kutokuosha gari kwa wakati (ndani na nje ya gari)

Kuosha gari kuna faida nyingi zaidi ya kuwa na muonekano mzuri. Kunaondoa kemikali amba-zo zinaweza kuleta uharibifu au kuoza kwa sehemu mbalimbali za gari. Inashauriwa gari lioshwe kila baada ya safari ndefu ili kuondoa majani na wadudu wanaoingia kwenye gari wakati wa kuendesha.

Gari lisiposafishwa ndani kwa muda mrefu kuna uwezekano michirizi ya vinywaji ikaingia kwenye vifaa vya gari na kuzuia utendaji wake.

Kutozingatia uvujaji wa mafuta

Ikiwa utaona aina yoyote ya mafuta yamemwagika chini ya gari lako ni ishara kuwa kuna tati-zo fulani. Mafuta yakiwa meusi au kahawia fahamu tatizo lipo kwe-nye injini na breki. Mafuta mekun-du ni tatizo la usukani. Ukiona hali ya namna hiyo ni muhimu kubaini tatizo na kurekebisha kwa wakati.

Columnist: mwananchi.co.tz