Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Ukatili wa kijinsia ni janga kwa taifa,Uzikwe

11920 Pic+ukatili tuwalinde watoto ni wetu sote

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

VITENDO vya ukatili vimezidi kujikita na kushamiri kila kukicha tofauti na hali ya mambo ilivyokuwakatika miaka ya nyuma.

Waathirika wakubwa wa vitendo hivi, ni watoto iwe katika familia zao kwa maana ya wazazi wao ama wanapokuwa chini ya uangalizi wa ndugu na jamaa zao.

Baadhi ya watoto ambao hukumbana na kadhia ya manyanyaso na kufanyiwa ukatili wa kijinsia katika familia, wakishaanza kupata akili, huamua kujitenga na kwenda kujitafutia mitaani bila kujali athari za uamuzi wao.

Hii imezalisha wimbi la watoto wasio na makazi rasmi, wakiishi katika mazingira hatarishi kiasi cha kupata matatizo makubwa zaidi ya kimalezi, ikiwemo kukutana tena na vitendo vya ukatili toka kwa wasiojua utu na hadhi ya wengine.

Watoto wengi wamekuwa waathirika wa vitendo vya kikatili kutokana na jamii waliyomo kukosa elimu bora ya kuwakinga watoto, japokuwa serikali imekuwa na jitihada kubwa ya kutoa elimu kwa jamii ya kwamba wajibu wa kumlinda mtoto, ni la kila mmoja kwa maana kuwa mtoto wa mwenzio ni wako.

Hata hivyo, kwa kiwango fulani masuala ya mila na desturi za baadhi ya jamii, yanachangia baadhi ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto kwa mfano ukeketaji pamoja na ndoa za utotoni.

UKEKETAJI

Kulingana na takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto UNICEF, ukeketaji unafanyika katika mataifa yasiyopungua 30, mengi yakiwa ya Afrika, Mashariki ya Kati na Asia.

Ukeketaji unamaanisha baadhi ya viungo vya sehemu za siri za msichana au mwanamke ama zinakatwa kwa sehemu fulani au zinanyofolewa kabisa na baadhi ya makabila, huwa wanashona sehemu hizo au kuzichanja.

Kwa upande wa Tanzania, ukeketaji ni moja mila na desturi kwa baadhi ya makabila, yakiwemo ya mkoa wa Mara.

Kimsingi, ni kitendo cha kinyama kwa mtoto wa kike kwani husababisha mtoto wa kike kuvuja damu nyingi na kuweza kupoteza maisha kabisa.

JUHUDI ZA SERIKALI

Serikali kwa upande wake imejitahidi kupaza sauti juu ya janga hili, lakini bado kuna watu wanadiriki kufanya huu unyama kwa sirisiri hasa vijijini hasa kwa baadhi ya makabila na mikoa kadhaa nchini.

Kwa upande mwingine, mbali ya ukeketaji pia suala la ndoa za utotoni, limekuwa ni tatizo kwa baadhi ya ya familia katika maeneo mengi nchini.

Watoto wengi wamekuwa wakilazimishwa kuolewa wakiwa katika umiri mdogo kwa kulazimika kukatisha masomo.

Mnamo Septemba, Mwaka 2019, Charles Mkojela (34), mkazi wa Mtumba, jijini Dodoma alihukumiwa kifungo cha miaka 30, kwa kosa la kumuoa mwanafunzi wa shule ya msingi.

Hii ni ishara ya kuonesha jinsi gani serikali inajitahidi kudhibiti ukatili kijinsia na kuwanyima watoto, kwani inawanyima haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Lakini, changamoto kubwa ni watu katika jamii kuwa waelewa na kuruhusu mabadiliko kwa kufanya vitendo sahihi kwa watoto hasa wazazi, pia wamekuwa wakichangia kushamiri kwa vitendo hivyo.

Aidha, uwepo wa imani potofu katika jamii hasa wa mfumo dume, pia imechangia kuleta ukatili wa kinjisia dhidi ya wanawake na watoto.

Kesi yingi zimekuwa zikihusishwa na masuala ya kishirikina ambapo baadhi ya wazazi ama ndugu wa karibu na watoto, wamekuwa wakishiriki vitendo hivyo vya kuangamiza watoto wasio na hatia.

Unaweza kukuta baba mzazi wa mtoto, anambaka mwanae wa kumzaa mwenyewe kwa kutekeleza maagizo ya mganga kwa madhumuni yao binafsi baada ya kufanganywa kuwa watapata utajiri kwa njia hiyo ya kishirikina.

Kuna mkasa mmoja, Mkoani Morogoro baba mmoja alimbaka mwanae wa kike wa mwaka mmoja na kuweza kusababisha kifo cha mtoto wake.

Huu sio tu ni ukatili uliopitiliza, pia ni unyama ambao unaakisi kuwapo kwa janga kubwa kwa kitaifa kwa nchi ya Tanzania kutokana na kukithiri kwa matukio ya ukatili dhidi ya watoto wenye haki ya kuishi na kulindwa.

WALIMU

Walimu mashuleni, pia wamekuwa wakichangia ongezeko la ukatili wa kinjinsia kwa baadhi yao kufikia hatua ya kuwabaka na kuwarubuni watoto kufanya ngono na baadhi ya Walimu, wamekuwa wakishiriki kuharibu maisha ya watoto.

Kitendo cha baadhi ya Walimu kujihusisha na vitendo hivyo, ni hofu nyingine kwa wazazi na walezi kwani kwa miaka mingi, imani yao ilikuwa kubwa zaidi kwa Walimu kutokana na asili na mazingira ya kazi yao, hasa ikizingatiwa ndio wanaokaa na mtoto kwa saa nyingi zaidi.

Hivyo, vitendo vya baadhi ya Walimu kujihusisha kuwa sehemu ya wanaowafanyia ukatili wa kingono watoto wa shule, inaondoa imani ya wazazi na walezi kwa Walimu kwa kuona baadhi yao, si mikono salama tena.

Mnamo Agosti mwaka 2019, wilayani Babati, Mkoani Manyara, Mwalimu Mkuu wa shule ya Rift Valley, Charles Msele, alidaiwa kuingia katika bweni la wanafunzi wavulana na kumlawiti mtoto wa umri wa miaka 11.

Kwa kosa la Mwalimu huyo dhidi ya mwanafunzi wa darasa la tano, Mahakama ya wilaya Babati, imemwadhibu kwa kifungo cha maisha.

SIRA YA KIMATAIFA

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto (UNICEF) ya mwaka 2017, wanawake na wasichana wapatao millioni 750 kote duniani waliolewa wakiwa chini ya umri wa miaka 18.

Kadhalika, taarifa hiyo inakadiria kuwa wasichana millioni 120 (mmoja kati ya wasichana 10), kote duniani wamekumbana na vitengo vya ukatili na uzalimishwa wa kingono bila ridhaa yao.

Kwa Tanzania, ni kati ya nchi zinazokabiliwa na tatizo la ukatili wa kijinsia na kwa muujibu wa twakimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu mwaka 2015/2016, inakadiriwa asilimia 40 ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15-49, wamefanyiwa uatili wa kupigwa au kingono katika maisha yao.

VISABABISHI

Mbali ya roho ya ukatili kwa wenye kujihusisha na vitendo hivyo, kwa upande mwingine kisababishi kingine cha hali hii, ni tamaa ya wahusika na kujikuta katika matatizo makubwa ya kufungwa miaka 30 kwa mujibu wa sheria.

Pamoja na uwepo wa adhabu hizo kali, baadhi ya mikoa imekithiri kwa vitendo vya ubakaji wa wanafuzi wa shule na kuwaharibia maisha yao.

Ni hivi karibuni, kijana mmoja aitwaye Ally Kibwe (20) wa Mkoani Rukwa, alihukumiwa kwenda jela miaka 50 na mahakama ya wilaya ya Nkasi kwa kosa la kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa darasa la tano.

MIKAKATI YA SERIKALI

Serikali kwa upande wake imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kupunguza ukatili wa kijinsia katika jamii ikiwemo kuongeza makali ya adhabu na mikakati mingine ya kitaifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Lengo hasa la Serikali, ni kuhakikisha vitendo vya ukatili vinapungua kwa kiwango cha asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Jinsia (2005), Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008); pamoja na Sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya mwaka 1998.

Kwa upande mwingine, kulingana na adhabu zinanzotolewa na serikali dhidi ya makosa ya ukatili wa kijinsia, ni kuwa fundisho kwa wenye kujihusisha na vitendo hivyo vya unyama kwa watoto kwa ujumla wake.

Hata hivyo, wananchi kwa upande wao wanashauriwa kusaidia harakati hizo kwa kupaza sauti pale wanapoona unyama ukifanyikwa kwani umoja ndio ukombozi, pia umoja na ushirikiano ni siraha ya mafanikio.

mwishooooo....

Columnist: www.tanzaniaweb.live